Na Saidi Mkabakuli, Kagera
Mkoa
wa Kagera na maeneo ya jirani wataanza kujivunia uwanja wa ndege wa
kisasa kufuatia kukamilika kwa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Akizungumza
na Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kagera, Mhandisi
Suleiman Athuman, amesema kwamba maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria
la kiwanja hicho upo kwenye hali nzuri na mkandarasi atabidhi kazi hiyo
mapema mwakani.
“Katika
mwaka wa fedha wa 2013/14 kazi zilizopangwa ni ukarabati na upanuzi wa
miundombinu ya kiwanja, ikijumuisha barabara ya kuruka na kutua ndege,
maegesho ya ndege, barabara ya kiungio, kwa sasa ujenzi unaendelea
vizuri na Mkandarasi atatukabidhi kazi mapema mwakani,” alisema Mhandisi
Athuman.
Akitoa
taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba, Mhandisi Mshauri
wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo amesema kuwa kazi za
usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege, ujenzi wa jengo jipya la
abiria na uzio wa usalama zimeshakamilika kwa asilimia 80.
“Kama
unavyojionea, sehemu kubwa ya kazi imekamilika, kwa makadirio ni zaidi
ya asilimia 80 ya ujenzi wa kiwanja hiki imeshakamilika,” aliongeza
Mhandisi Gobolo.
Kwa
mujibu wa mpangokazi wa ujenzi wa kiwanja hicho hadi kufikia mwezi Juni
2014, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa
barabara ya kuruka na kutua ndege, barabara ya kiungio na maegesho ya
ndege kwa kiwango cha lami; na ujenzi wa jingo jipya la abiria kufikia
hatua ya usimikaji wa paa na mifumo ya maji safi, maji taka na umeme; na
kuendelea kwa ujenzi wa jengo la abiria na kituo cha umeme.
Naye,
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amesema kuwa Serikali imeazimia
kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege hususan miradi
iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa.
“Kwa
mujibu Programu ya Matokeo Makubwa Sasa, serikali kupitia Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege nchini ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza viwanja vya
ndege vyote ili viwe na kiwango kizuri kwa watumiaji wa viwanja hivyo,”
alisema Bibi Mwanri.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakiwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kagera kujionea maendeleo ya
Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja hicho. Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Meneja Mradi wa Upanuzi wa
Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Katikati) na
Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia).
Ujenzi unaendelea! Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kagera.
Mhandisi
Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo akitoa maelezo
ya namna ya kiwanja hicho kitakavyoonekana mara kitakapokamilika.
Pichani ni muonekano mpya wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Wahandisi
Pius Gobolo (kushoto), (Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege
cha Bukoba) na Suleiman Athuman (watatu kulia), Meneja Mradi wa Upanuzi
wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba wakitoa maelezo mara walipoingia kwenye
sehemu ya abiria ya jengo jipya la kiwanja hicho.
Meneja
wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia) akifafanua jambo kwa
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wanaoshuhudia ni
Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi
Suleiman Athuman (Wapili kushoto) na Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa
kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo (Kushoto).
Hadi
kuleeee.. Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Mbele)
akimuonesha Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia) sehemu
inayopendekezwa kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipangoimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango ikiendelea na kazi ya ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha
Bukoba.
PICHA NA SAIDI MKABAKULI
No comments:
Post a Comment