Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro (kushoto) na afisa uhamiaji mkoa wa Njombe Rose Mhagama wakiwa kituoni hapo.
Afisa uhamiaji mkoa wa Njombe Rose Mhagama akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa kituo cha Nyumba ya yatima Bulongwa
Mkuu wa wilaya akifurahia jambo
Watoto yatima wakipewa zawadi na Idara ya uhamiaji mkoa wa Njombe
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa kituo cha Nyumba ya yatima Bulongwa
Baadhi ya msaada uliotolewa
Mkuu wa wilaya akikabidhiwa msaada huo na afisa uhamiaji mkoa wa Njombe
Afisa Uhamiaji mkoa wa Njombe akisema mawili matatu
akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima
Mkuu wa wilaya katika picha ya pamoja na watoto yatima
Hivi
karibuni Idara ya uhamiaji mkoa wa Njombe iliunga mkono jitihada za mkuu
wa wilaya ya makete Josephine Matiro kusaidia vituo vya watoto yatima
wilayani humo kwa kutoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 1
Akizungumza
wakati akikabidhi msaada wao afisa uhamiaji mkoa wa Njombe Rose Mhagama
alisema wameguswa na suala hilo na kuamua kuvisaidia vituo vya watoto
yatima Makete vitu mbalimbali, na kuwaomba wadau wengine kujitokeza
kuwasaidia watoto hao
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya Hiyo Bi Josephine matiro amewataka wanamakete
kubadilika na kuacha dhana kuwa watoto hao watasaidiwa na wafadhili
kutoka nje na badala yake nao wawasaidie watoto hao kwa kitu chochote
walichojaliwa na Mungu
Vituo vilivyonufaika ni Nyumba ya yatima Bulongwa, Fema Matamba na Kituo kipya cha Kisinga
Na Edwin Moshi wa eddy blog
No comments:
Post a Comment