Matukio Bungeni : Spika wa Bunge Anne Makinda Asitisha Bunge mara baada ya kutokea Sintofahamu wakati wa mjadala wa sakata la ESCROW - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 29 November 2014

Matukio Bungeni : Spika wa Bunge Anne Makinda Asitisha Bunge mara baada ya kutokea Sintofahamu wakati wa mjadala wa sakata la ESCROW


Sintofahamu iliyotokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma Ijumaa Novemba 28, 2014 imepelekea Spika Anne Makinda (pichani) kulazimika kusitisha shughuli za Bunge mpaka hapo watapojadiliana tena. Hii ni baada ya majadiliano makali kuhusu kuwajibishwa ama la kwa viongozi wanaohusika na sakata la akaunti ya Escrow. Hali hii iliibuka baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA na kambi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe kuinuka na kusema kuwa Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, na kwamba kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kutoka maamuzi kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. Kwa maelezo zaidi Bofya hapa >>>

No comments:

Post a Comment