Matukio :Tanzania yachukua Rasmi Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika mashariki - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 29 November 2014

Matukio :Tanzania yachukua Rasmi Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika mashariki


Tanzania leo imekabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki baada ya Kenya kumaliza muda wake wa kipindi cha mwaka mmoja.Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta na Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo walipokea Uenyekiti huo katika Mkutano wa Baraza wa Mawaziri uliofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC), Jijini Nairobi, Kenya. Rais wa Tanzania anatarajiwa kupokea Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki siku ya Jumapili katika Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya utakaofanyika pia hapa KICC.

No comments:

Post a Comment