Serikali
ya Jamuhuri ya Watu wa China imekusudia kuongeza nguvu za ziada katika
kusaidia kuimarisha miundo mbinu ndani ya Bara la Afrika kwa lengo la
kuyajengea uwezo wa uzalishaji wa kiuchumi Mataifa mbali mbali yaliyomo
ndani ya Bara hilo.
Kauli
hiyo imetolewa na Makamu wa China Bwana Li Yuanchao wakati yeye na
ujumbe wake alipofanya mazungumzo Rasmi na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiuongoza Ujumbe wa Zanzibar kwa Niaba ya
Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Bararaza la Mapinduzi Dr. Ali Moh’d
Shein hapo hoteli ya La gema Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Bwana
Li Yanchao akiwa Zanzibar kwa siku moja akiendelea na ziara yake ya siku
sita Nchini Tanzania alisema katika utekelezaji wa azma hiyo China
imejipangia kutumia Yuan Bilioni 2.2 katika mipango yake ya kuimarisha
miundo mbinu hiyo ya uwekezaji kwenye sekta ya biashara.
Aliishauri
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuitumia fursa hiyo adhimu kwa
kuchagua miradi yake itakayoipa kipaumbele cha kwanza kwa kuwasiliana na
Ofisi ya Ubalozi mdogo wa Nchi hiyo uliopo Zanzibar ili kuratibu miradi
hiyo na hatimae hatua za utekelezaji zianze mara moja.
Naye
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa shukrani
zake alisema Zanzibar itaendelea kuiheshimu na kuithamini China kutokana
na msimamo wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati za
kuimarisha uchumi.
Balozi
Seif alieleza kwamba Jamuhuri ya Watu wa China inastahiki kupongezwa
kwa misaada yake mikubwa inayotoa kwa Zanzibar ambayo haijawahi kutokea
katika Historia ya Zanzibar tokea Mapinduzi ya Mwaka 1964.
Alisema
Wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakishuhudia misaada tofauti inayotolewa
na China ndani ya kipindi cha miaka 50 tokea Mapinduzi iliyolenga katika
sekta za afya, elimu, maji, miundo mbinu, kilimo pamoja na mawasiliano.
Bwana
Christopher Mush Smith wa Hoteli ya La Gema akikata Keki Maalum yenye
Bendera za Tanzania na China iliyoandaliwa na Hoteli hiyo kwa ajili ya
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Li
Yuanchao aliyepo pembeni yake akiwa sambamba na Mwenyeji wake Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu
wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao akipongeza na Mwenyeji wake Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya
mazungumzo yaop yaliyofanyika katika Hoteli ya La Gema Nungwi Mkoa wa
Kaskazini Unguja.
Balozi
Seif na Mgeni wake Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao wakitoa
nje ya ukumbi baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyoshirikisha viongozi
wa ngazi za juu wa pande zote mbili.
Bwana
Li Yuanchao upande wa kushoto alinyanyuka na kufurahia muziki murua
uliokua ukiporomoshwa na Kikundi cha taadab asilia cha Akheri Zamani
wakati wa tafrija yao kwenye Hoteli ya La Gema Nungwi.
Ujumbe
wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif ukiendelea na mazungumzo yao na ujumbe wa China chini ya Makamu wa
Rais wa Nchi hiyo Bwana Li Yuanchao hapo katika ukumbi wa Hoteli ya La
Gema Nungwi.
Balozi
Seif na mgeni wake Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao
wakifuatilia muziki laini wa kikunci cha taarabu asilia cha Akheri
Zamani hakipo pichani kwenye tafrija yao hapo La Gema Nungwi.
Ukumbi
wa Hoteli ya La Gema Nungwi iliyopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja
ulisheheni vionja vya muziki wa Taarab asilia ya kikundi cha Akheri
Zamani wakati wa tafrija maalum kwa ajili ya ugeni wa Serikali ya China
uliooongozwa na Makamu wa Rais wa Nchi hiyo Bwana Li Yuanchao.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment