NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE : JAMES OLE MILLYA AFUNGA PINGU ZA MAISHA, CHRISTINA SHUSHO NA SOLOMON MUKUBWA WATUMBUIZA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 8 May 2014

NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE : JAMES OLE MILLYA AFUNGA PINGU ZA MAISHA, CHRISTINA SHUSHO NA SOLOMON MUKUBWA WATUMBUIZA

Kamanda James Ole Millya na Bi. Janeth  wakipata picha na wadau katika sherehe ya harusi yao iliyofanyika katika viwanja vya Bortanical Garden, Sakina, Jijini Arusha.
Mwimbaji toka Kenya Solomon Mkubwa alitumbuiza kumuunga mkono Milya
Mdau mkubwa wa blog hii, akipata ukodak na Bw na Bi. James Ole Millya Jijini Arusha
Mhe. Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini akilishwa keki ya Heshima
Mr and Mrs Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini
Mh. Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa nae alimuunga mkono kijana Milya
Mhe. Freeman Mbowe akiteta na mdau wa blog ya Wazalendo 25 Blog Bw. Daniel Urioh anaetarajia kuwa diwani wa kata ya Olasiti, akiambiwa "Pambana na Utashinda".
Bw. Elipokea Urio na James Milya (Classmates)
Christina Shusho akiwapagawisha wageni waalikwa kwa nyimbo za Injili katika sherehe za ndoa ya James Ole Millya

Sherehe ya kusindikiza harusi ya James Ole Millya na mkewe Bi Janeth ilikuwa ya kipekee kwa namna mbalimbali ukiachana na idadi kubwa ya watu waliohudhuria.
Ni sherehe iliyokuwa na mbwembwe za kila namna na vikorombwezo chungu tele.

Utani wa kisiasa baina ya Chadema anakotoka bwana harusi na CCM anakotoka bi harusi ulikuwa ni kivutio tosha kwa waliohudhuria. Makundi ya vyama vyote yakiwa na viongozi wao wakubwa yalikuwa yakitambiana kwa kushangilia kila walipopata fursa toka kwa MC. Mabaraza ya vijana kwa vyama vyote ndio yaliyotia for a kwa pande zote katika kutambiana. Huku CCM wakiimba “CCM..CCM..” wenzao wa Chadema walikuwa wakionyesha ishara ya vidole vitatu na kuimba “UKAWA…UKAWA” kila alipotambulishwa kiongozi wao ama kuitwa kufanya jambo fulani. Bavicha Arusha waliongozwa na Mwenyekiti wao Noel Olevaroya na Katibu Glory Kaaya.

Kulikuwa na idadi kubwa ya viongozi wa kitaifa na kisiasa. Alikuwepo Mwenyekiti wa Chadema Taifa ambaye pia ni mbunge wa Hai, Mh Freeman Mbowe bila kumsahau Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema na Mh Kihwelu kwa Upande wa Chadema. Walikuwepo pia Mwenyekiti wa CCM  Arusha Mh Olenangoye na Mbunge Viti Maalum CCM Mh Catherine Magige. Madiwani Kessy wa Kaloleni, Ally Bananga wa Sombetini na Msofe wa Daraja mbili wote kupitia Chadema walihudhuria.

Viongozi wa kiserikali alikuwepo Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja Kota, bila kumsahahu Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini John Mongela. Mbunge wa Simanjiro anakotokea James Millya, Mh James Ole Sendeka hakuonekana ukumbini hapo pamoja na kuwa alialikwa. Blog hii iliweza kufahamu kuwa takribani watu 10 walialikwa kutoka katika kila kijiji cha Wilaya ya Simanjiro, pengine ndio sababu iliyopelekea James kupewa zawadi ya ng’ombe wengi mno kutoka kwa jamaa zake Maasai.

Upekee haukuishia hapo tu kwani kwa upade wa washereheshaji walikuwepo nguli wawili wa fani hiyo, MC OJ (Alezander Josephat Ole Miidimu Sirkion) ambaye ni mchekeshaji kutoka Kenya na aliwahi kuwa Kampeni Meneja wa Raila Odinga, bila kumsahau Godwin Gondwe kutoka Tanzania.

Burudani haikuishia hapo kwani nyimbo za injili ziliimbwa na wasanii Christina Shusho kutoka Tanzania na Solomoni Mukubwa kutoka Kenya ambao kwa pamoja walikonga nyoyo za wahudhuriaji vilivyo.

No comments:

Post a Comment