Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokewa kwenye
uwanja wa ndege wa Arusha na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande
Othman kwa ajili ya Kufunga Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake
Duniani {IAWJ } unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Arusha { AICC }. Nyuma ya Mh. Chande ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu.
Jaji
Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu akimkaribisha Balozi Seif
kwenye uwanja wa ndege wa Arusha Jioni kwa ajili ya kuufunga Mkutano wa
Majaji wanawake Duiniani. Nyuma ya Jaji Makungu ni Jaji Mfawidhi wa Mahkama Kuu ta Tanzania Kanda ya Arusha Mh.Stella Mugasha.
alozi
Seif na Mwenyeji wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman
wakitoka nje ya uwanja wa ndege wa Arusha kuelekea Hoteli kwa mapumziko
kabla ya kuhudhuria Ufungaji wa Mkutano wa Kimataifa wa Majaji wanawake
Duniani hapo Ukumbi wa AICC. Kati kati yao ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Seif Iddi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipokea muhtasari wa Ratiba itakayomkabili
wakati wa hafla ya Ufungaji wa Mkutano wa Kimataifa wa Majaji Wanawake
Duniani { IAWJ } mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Kimataifa ya
Naura Spring kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mhamed Chande Othman kushoto yake. Kulia
ya Balozi Seif ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu na Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha Mh. Stella Mugash.
Wajumbe
wa Mkutano wa Kimataifa wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani { IAWJ }
wakiangalia ngoma za Utamaduni waliyoishuhudia wakati wa matembezi yao
ya mapumziko ya usiku kwenye kituo cha Utamaduni Mjini Arusha.
No comments:
Post a Comment