Mkurugenzi Mkuu wa
Helvetic Solar Contractors Eng. Patrick Ngowi akiwa na mwenyeji wake
Mkurugenzi Mkuu wa IPP Media Bi. Joyce Mhavile alipofika katika ofisi
hizo mapema leo kwa ajili ya mazungumzo na kuhojiwa katika kipindi cha
Business Edition, kitakachorushwa Ijumaa hii saa 2 na dakika 45 usiku,
Capital TV.
Dar es Salaam. 21 Mei, 2013. Mkurugenzi Mkuu wa Helvetic Solar Contractors Eng. Patrick Ngowi ameendelea kutoa rai kwa vijana nchini Tanzania kuwa na moyo na bidii ili kuweza kutimiza ndoto zao za maendeleo na kujikwamua kiuchumi. Eng. Ngowi ambaye pia ni mshindi
wa ‘Forbes 2013: 30 under 30: Africa’s Best Young Entrepreneurs’ alisema maneno hayo mapema leo katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa IPP media Bi. Joyce Mhavile alipofika kufanya ziara na mahojiano maalum katika kituo hicho.
“Vijana wa kitanzania wanafursa nyingi sana katika nchi yetu, imefika wakati sasa vijana wajitambue kwamba wanaweza kutimiza ndoto zao kadiri bidii zao zitakavyowatuma. Kwa mfano, mi nilianza na mtaji wa shilingi milioni mbili, lakini hivi sasa nilipofikia biashara yangu imekua na nimeweza kufanya maajabu makubwa katika soko ukizungumzia
swala ya nishati ya jua,” alisema Eng. Ngowi.
Aliongeza, “Kinachotakiwa ni kuwa mbunifu katika biashara unayofanya, kuwa na ujasiri pamoja na umakini wa kile unachokipenda na pale unapotaka kufika. Yote yanawezekana na kijana yeyote anaweza fanikiwa.”
Pamoja na hayo Eng.
Ngowi aliwapongeza sana IPP media kwa mafanikio yao waliyopata katika
kipindi chote tangu kianzishwe, ikiwemo tuzo ya ‘Number 1 Super Brand’
katika Afrika Mashariki hivi karibuni.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa IPP Media Bi. Joyce Mhavile alimpongeza kwa mafanikio yake na kumshukuru sana Eng. Ngowi kwa ugeni wake.
Africa’s Best Young Entrepreneurs’. Picha na habari na Amani Nkurlu.
No comments:
Post a Comment