Inspector Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi. |
Ushawishi ukiendelea. |
Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama. |
Nje ya Mahakama kuelekea lango kuu. |
Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama. |
Mashuhuda. |
Tukio hilo limetokea majira ya saa 4:00 tarehe 7,Mei/2014 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati
mahabusu hao walipofikishwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao,
lakini ghafla walipofika kwenye viwanja vya mahakama hiyo walitimua
mbiyo kuelekea kwenye mlingoti wa Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo.
Wananchi
waliokuwa katika viwanja vya mahakamani hapo waliachwa midomo wazi na
hali ya mshangao, mara baada ya mmoja kati ya hao wawili wakifanikiwa
kuufikia mlingoti huo na kuvua nguo kisha kuanza kupiga kelele kwa
kupaza sauti kudai haki itendeke.
Tukio
hilo pia lilishuhudiwa na watumishi wa Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya
Mwanzo, Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka ya jijini hapa (MWAUWASA),
Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), na taasisi zingine zilizo jirani na
majengo ya mahakamani hapo na wananchi waliokuwa wakisubilia kesi zao
kutajwa.
Mahabusu
hao sita waliojaribu kutoroka na kuishia kudhibitiwa vyombo vya dola,
walitajwa kwa majina kuwa ni Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo
zote na kubaki mtupu eneo la mlingoti wa Bendera ya Taifa, ambaye
anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012.
Watuhumiwa
wengine waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro
(35), Marwa Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na mwingine ambaye
hakufahamika majina yake mara moja, wote wanakabiliwa na kesi ya Jinai
Na. 215/2013 na walikamatwa tangu mwaka 2011.
Wakiwa
katika viwanja vya mahakama hiyo baada ya kudhibitiwa na askari polisi,
mmoja wa mahabusu hao walisikika wakisema: “Haiwezekani, tangu mwaka
2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa. Wengine
tumebambikiziwa kesi. “Tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie tumekaa
muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011 tulipo
kamatwa tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe”.
Baada
ya malalamiko yao, ndipo askari mmoja aliyejitambulisha kuwa ni
Inspekta Henry akiwa na wenzake sita waliokuwa wakiwadhibiti wasikimbie
na kuwahoji kuhusiana na madai yao, huku askari hao wakiwataka kuondoka
katika mlingoti huo na kumtaka Warioba avae nguo ili waweze kuingia
mahakamani.
“Pamoja
na maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili ni kosa
jingine la jinai, hivyo ni vema mkaondoka kwenye mlingoti huu na kuingia
mahakamani. Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa,” alisema
Inspekta Henry.
Mmoja
wa maofisa waandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza,
ambaye alikataa kutajwa jina lake, alidai ushahidi wa kesi za watuhumiwa
hao bado haujakamilika, na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa na
mahakama ya wilaya kwani haina uwezo na badala yake zitatajwa tu kisha
kuhamishiwa Mahakama Kuu.
“Bado
hiyo ni Criminal Case (kesi ya mauaji) au PI Case hivyo Mahakama Kuu
haiwezi kuzungumzia hilo kwa sasa kwa kuwa utaratibu wa mahakama kuu
ikisha kuwa tayari huitwa ‘Criminary Session Case’, ambapo sasa
hupangiwa namba ya kesi na Jaji wa kuisikiliza,” alisema. Pcha zote na Gsengo Blog
No comments:
Post a Comment