SAY NO TO RACISM, SEMA HAPANA KWA UBAGUZI: WAHARIRI NA WAANDISHI WAPINGA VITENDO VYA UBAGUZI KWA WACHEZAJI WAAFRIKA WANAOCHEZA SOKA LA KULIPWA ULAYA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


30 Apr 2014

SAY NO TO RACISM, SEMA HAPANA KWA UBAGUZI: WAHARIRI NA WAANDISHI WAPINGA VITENDO VYA UBAGUZI KWA WACHEZAJI WAAFRIKA WANAOCHEZA SOKA LA KULIPWA ULAYA

 NI MCHEZAJI WA BARCELONA ALIYERUSHIWA NDIZI NA KISHA AKAIOKOTA NA KUIMENYA NA KISHA KUILA.  
Baadhi ya wahariri na waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The African, Mwani Nyangasa na wenzake wakila Ndizi kwa pamoja kama ishara ya kumuunga mkono mchezaji wa Barcelona Daniwl Alves, ambaye ni Mwafrika aliyeonyeshwa vitendo vya ubaguzi wa rangi hivi juzi wakati akiwa mchezoni na timu yake ilipokuwa ikicheza na Villarreal ya Hispania, ambao mashabiki walimrushia ndizi mbivu uwanjani wakimaanisha kumfananisha na Nyani na yeye kwa kuwaonyesha kuwa hajali kitendo hicho aliiokota na kuimenya na kisha kuanza kuila, jambo ambalo liliungwa mkono na wengi na kumpongeza kwa kitendo chake cha ujasiri, na kuendelea na mchezo.
Baloteli pia ni mmoja kati ya wachezaji Waafrika aliyeunga mkono kitendo cha mwafrika mwenzake kuwakebehi na kuwadharau mashabiki hao wa ubaguzi. Na pia Baloteli ni mmoja kati ya wachezaji wanaokumbana na vitendo hivyo vya unyanyasaji uwanjani mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad