Na Waaandishi wetu , hudumabongo@gmail.com
Kampuni
ya mawasiliano ya simu za mkononi, Tigo imeshikilia usukani wa biashara
inayoongoza kwa kero kwa wateja baada ya kuibuka kuwa mshindi miongoni mwa
biashara 31 zenye kero kwa wateja nchini
.
Taarifa
hii ni matokeo ya zoezi linaloendeshwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii ya
Twitter na Facebook wenye lengo la kuboresha sekta binfasi nchini Tanzania hususani
huduma kwa wateja.
Nafasi
ya pili inashikiliwa na Shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO mkoa wa Dar es
Salaam ambao katika mzunguko wa kwanza ndiyo walishikilia usukani wa kero.
Wakiongoza kwa kero ya kukata umeme bila taarifa kitu kinadaiwa kuwa ni mgao.
Nafasi
ya tatu imeendelea kushikiliwa na Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya
Vodacom ambayo imeendelea kushika nafasi hiyo katika mzunguko wa pili.
Hakukuwa
na mabadiliko katika makundi mengine mfano huduma za usafiri wa anga ambapo
mshindi amebakia kuwa ni Precision Air, huku katika huduma za kibenki
zikiendelea kushikiliwa na benki ya CRDB.
Huduma
za ving’amuzi vya kulipia vyenye kero imeendelea kushikiliwa na Star Times waliopata kura 4 za ziada ukilinganisha na
matokeo ya mzunguko wa kwanza.
Katika
mzunguko huu biashara mbili zaidi ziliingia katika kinyanganyiro hicho ambao ni
Kampuni mpya ya huduma za ndege ya Fast Jet na Dalalada inayofanya safari kati
ya Mwenge na Kariakoo yenye nambari za usajili T 868 BHU.
Haya
ni maoni ya wateja wa huduma hizi yaliyokusanywa kupitia akaunti ya twitter
@hudumambayatz na Facebook group ya HUDUMA BONGO ambapo jumla ya kero 174 ziliwasilishwa na wateja
toka mchuano uanze.
Zoezi
la kukusanya maoni haya linaendelea katika mzunguko wa tatu ambapo kauli mbiu
ya ni “Sisi ndio waajiri wenu , huduma bora ni haki yetu”. Kero katika huduma
na bidhaa mbalimbali za kulipia mfano afya, elimu, usafiri, benki, mawasiliano
zinapokelewa na kutafutiwa suluhisho kwa maendeleo ya taifa letu.
Kwa
maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kura na zoezi hili linavyofanyika tembelea
link ifuatayo http://bit.ly/10SARH1 |
Habari : Kazi ya bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) ni kulea
Waandishi- Prof. KABUDI
-
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Bw.
Patrick Kipangula akitoa neno mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaana
Michez...
4 hours ago
No comments:
Post a Comment