AFYA ZETU :MHE. GHARIB BILAL AHUDHURIA KWENY MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


30 Apr 2014

AFYA ZETU :MHE. GHARIB BILAL AHUDHURIA KWENY MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kuhutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na Afya Duniani.
Afisa mkuu mwandamizi wa mazingira katika mamlaka ya Bandari Thobias Sonda akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, juu ya utumiaji wa vifaa vya kupimia hewa, wakati alipotembelea Banda la maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mtaalam wa uchunguzi wa vyakula katika maabara ya mkemia mkuu wa Serikali Edith Wilbald akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipotembelea Banda la maabara ya uchunguzi wa vyakula kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mtaalam wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Noth Mara Gold Mine Paul Kagodi akimuonesha Makamu wa Rais vifaa vinavyotumika katika kazi ya uchimbaji wa madini wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad