Mkurugenzi wa Lino
International Agency, Hashim Lundenga (katikati) akiwa na Redds Miss
Tanzania 2012 Brigitte Alfred (kulia) na Miss Tanzania wa sasa Happiness
Watimanywa wakati wa sherehe ya Kumpongeza (Brigitte) kwa kushinda nafasi
ya tatu ya taji la dunia la kipengele cha urembo wenye malengo maalum.
Mrembo huyo aliwashinda warembo 127.Sherehe hiyo ilifanyika kwenye hotel
ya Giraffe Ocean mwishoni mwa wiki.
*******
Mwandishi wetu
Redds Miss Tanzania
2012, Brigitte Alfred Lyimo amesema kuwa ushindi wake wa nafasi ya tatu
katika kipengele cha urembo wenye malengo maalum katika mashindano ya
Miss World mwaka huu ni wa Watanzania wote.
Brigitte alisema hayo
katika hafla ya kuagwa iliyoandaliwa na waandaaji wa mashindano ya
urembo nchini, kampuni ya Lino International Agency iliyofanyika kwenye
hotel ya Giraffe.
Alisema kuwa
amefarijika sana kushinda nafasi hiyo kwani ilishirikisha warembo wote
walioshindana mwaka huu katika mashindano hayo. Alisema kuwa hakuwa kazi
rahis kushika nafasi hiyo kwani kipengele hicho ushirikisha warembo
wote.
“Namshukuru mama yangu, Verdiana
Mashingia ambaye alikuwa bega kwa began a mimi katika kuhakikisha mradi
wangu wa ujenzi wa bweni la albino wa shule ya smingi Buhangija
shinyanga unafanikiwa, pongezi pia kwa kamati ya Miss Tanzania na
wadhamini, Redds,” alisema Brigitte.
"Ndoto zangu za
kuitumikia jamii hazitaishia hapa, nitaitumikia na nitaendelea
kuwasaidia Albino ambao wamenichagua kuwa barozi wao," alisema mrembo
huyo.
Aidha Brigitte
alimpongeza Hapiness na kumtaka atumie kipaji alichonacho na urembo wake
wa asili kuitoa kimasomaso Tanzania kwenye mashindano ya mwakani.
Mkurugenzi wa Lino
International Agency, Hashim “Uncle” Lundenga alisema kuwa Brigitte
amefanya kitu cha kihistoria Tanzania na kuzishinda nchi kubwa mbali
mbali kama Uingereza, Ufaransa na nyingine nyingi.
Lundenga alisema kuwa
wamefarijika kwa mafanikio hayo na ndiyo maana wameamua kufanya hafla
hiyo ambayo ni ya kihistoria huku akiwapongeza wadhamini, Redds kwa
kudhamini hafla hiyo.
Alisema kuwa ni
vigumu kuamini, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa fai yao inazidi
kukuwa, tena kwa mafanikio tofauti na watu wanavyodhani.
“Mfano mzuri ni mama
yake Brigitte alivyokuwa bega kwa bega wakati wote mwanaye alivyokuwa na
taji, huu ni mfano wa kuigwa na tunaomba wazazi wafuate nyayo za mama
huyu,” alisema Lundenga.
Lundenga alisema kuwa
Brigitte ameleta changamoto kubwa kwa mrembo wa sasa Happiness
Watimanywa katika mashindano yanayofuata ya urembo ya dunia.
"Brigitte amefanya
vizuri japo hakufanikiwa kutwaa taji la dunia, kuwa namba tatu kwenye
taji la mrembo mwenye malengo ambalo kuacha taji la dunia ili
linafuatia, Brigitte anahitaji kupongezwa," alisema.
Alisema kuwa Brigitte
ameonyesha ushujaa na kuwapita warembo kutoka mataifa makubwa dunia
ambao walichuana kwenye mashindano hayo na yeye kufanikiwa kuingia hatua
ya tatu bora kwenye taji hilo.
No comments:
Post a Comment