MSANII WA HIP HOP WA ARUSHA 'JCB' AFUNGA PINGU ZA MAISHA . - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Feb 2013

MSANII WA HIP HOP WA ARUSHA 'JCB' AFUNGA PINGU ZA MAISHA .

JCB akiwa na mkewe Diana wakati wa kusaini vitabu vya ndoa.
 Msanii wa miondoko ya hip hop kutoka A City - Arusha a.k.a JCB Makalla ameuaga ukapera juzi kati, baada ya kufunga pingu za maisha na mwana dada Diana.

JCB akizungumza na Asili Yetu Tanzania blog pamoja na Wazalendo 25 blog jana majira ya  jioni, msanii huyu alikiri kufunga ndoa na kipenzi chake ambae tayari walikuwa wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume anayekwenda kwa jina la Albert 'JCB' Makalla.


Diana mke wa JCB akidondoka  sahihi katika kitabu cha ndoa ili kuihakikishia dunia kuwa yeye ni mwili mmoja na JCB Makalla.
JCB nae akianguka sahihi katika kitabu cha kuandikisha ndoa ,ili kuihakikishia dunia kuwa yeye ni mwili mmoja na Diana 'JCB' Makalla.
JCB akiwa na mke wake DIANA
 Ndugu Jamaa na marafiki waliohudhuria tukio hilo zuri la kihistoria. Mkurugenzi wa blogu ya Wazalendo 25 anawatakia maisha mema na yenye utulivu katika ndoa yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad