DIONIS MALINZI AIKABIDHI TAIFA STARS BENDERA YA TAIFA, AZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA USHINDI - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 8 November 2011

DIONIS MALINZI AIKABIDHI TAIFA STARS BENDERA YA TAIFA, AZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA USHINDI

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi akishikana mkono na kocha mkuu wa timu ya taifa Taifa Strs Jan Paulsen, mara baada ya kumkabidhi rasmi bendera ya taifa Henry Joseph ambaye ni kapteni wa timu hiyo, katika hafla ya kuiaaga timu hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa Jana jioni, kulia ni mene3ja wa timu hiyo Bw. Mutebezi.
Taifa Stars inadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Seregeti Lager kwa muda mrefu sasa na timu hiyo imeonyesha mafanikio kwa kiwango kikubwa tofauti na hapo awali ilipokuwa haina udhamini.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi akizungumza na wachezaji viongozi wa TFF pamoja na wadau mbalimbali, waliohudhuria katika hafla hiyo jana.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Leodger Tenga akizungumza katika hafla hiyo jana.
Kocha Mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars Jan Paulsen akizungumza katika hafla hiyo ambapo aliahidi kuwa, timu yake itafanya kazi kuwabwa kuhakikisha inaondoka na Ushindi huko Chad.
Mkurugenzi wa Mahusiano Kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda akizungumza kwa niaba ya kampuni ya bia ya Serengeti katika hafla hiyo.
Golikipa wa timu ya Taifa Stars Juma Kaseja akipiga ngoma huku wanenguaji wa kundi la Wanne Star wakicheza wakati wa hafla ya kuwapongeza.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi wa pili kutoka kushoto na mkurugenziw aMahusiano (SBL) Teddy Mapunda kushoto pamoja na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Leodger Tenga wa pili kutoka kulia wakiangalia kwa makini tangazo jipya linalohamasisha ushindi kwa timu ya Tanzania Taifa Stars, kulia ni Mjumbe wa BMT Juma Pinto.
Mkurugenzi wa Mahusiano Kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda akiongozana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi, kuelekea ukumbini kwa ajili ya kuwaaga wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars, nyuma kulia ni Golikipa wa timu hiyo Juma Kaseja.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini BMT Bw. Dionis Malinzi kulia na mkurugenzi wa Mahusiano SBL Teddy Mapunda wa pili kutoka kushoto, pamoja na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Leodger Tenga katikati wakifuatilia jambo katika hafla hiyo , kulia ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars Jan Paulsen.
Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akizungumza katika hafla hiyo kumkaribisha Mkurugenzi wa Mahusiano Teddy Mapunda.
Mwanamuziki na Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiteta jambo na golikipa wa tim u ya Tifa Stars Juma Kaseja.
Wadau kutoka kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakishoo Love katika hafla hiyo.
Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa Stars na Kocha mkuu wa timu hiyo Jan Paulsen. 
Na Full shangwe Blog

No comments:

Post a Comment