Utamaduni : Rais Samia Atembelea Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Songea Mkoani Ruvuma - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Monday, 23 September 2024

Utamaduni : Rais Samia Atembelea Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Songea Mkoani Ruvuma






Matukio mbalimbali wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Songea mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Songea mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi wakati akielekea Songea mjini wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la pamoja la Mashujaa wa Vita vya Majimaji walionyongwa na Wajerumani tarehe 27/02/1906 wakati wa Vita hivyo mjini Songea. Rais Dkt. Samia ameanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ambapo atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoka kwenye moja ya nyumba ya utamaduni wa asili ya Wangoni iliyopo katika Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Songea mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024. 

No comments:

Post a Comment