Matukio : Mhe. Mizengo Pinda Asisitiza Uwazi katika Matumizi ya Takwimu Sahihi - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


28 Apr 2015

Matukio : Mhe. Mizengo Pinda Asisitiza Uwazi katika Matumizi ya Takwimu Sahihi

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akifungua Kongamano la Kimataifa la Siku 3 la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa awali akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika waliohudhuria Kongamano la Siku 3 la Kimataifa kujadili Matumizi ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair akizungumza kabla ya uzinduzi wa  Kongamano  la Kimataifa la masuala ya Takwimu la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa  kutoka Afrika na nje ya Afrika.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizindua kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kushoto kwa Waziri Mkuu na Prof. Ben Kiregyeza (kulia) ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hicho.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akionyesha kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akionyesha kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Waziri Mkuu akizungumza akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi za Takwimu kutoka  nchi 32 za Afrika na 18 za nje ya Bara la Afrika waliohudhuria Mkutano wa siku 3 wa Takwimu  jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu akizungumza jambo na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bi. Irena Krizman leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua kongamano la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika. Katikati ni mjumbe kutoka Afrika ya Kusini Bw. Pali Lihohla.
Waziri Mkuu akizungumza akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua  kongamano la Kimataifa la Wakuu wa Taasisi za Takwimu kutoka  nchi 32 za Afrika na 18 za nje ya Bara la Afrika.
Waziri Mkuu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua  kongamano la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 32 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika.(Picha na Aron Msigwa Maelezo )

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad