Bana ya shoo hiyo ya Gusagusa Min band na Asia Idarous Khamsin itakayofanyika nchini Uingereza
London, Uingereza
Mbunifu
wa mavazi nchini ‘Mama wa Mitindo’, Asia Idarous Khamsin yupo nchini
Uingereza akiwa ameambatana na magwiji wa muziki wa taarab kutoka
Tanzania, Gusagusa Min Band ambao watafanya maonyesho makubwa ndani ya
miji ya nchi hiyo ikiwemo London na Northampton.
Kwa
mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo nchini humo, Kampuni ya Didas
Entertainment ya Uingereza walieleza kuwa, shoo ya kwanza itakuwa Mei 2,
katika viunga vya mji wa London na shoo nyingine ni Mei 3 katika mji wa
Northampton ambapo kutakuwa na fashion shoo ‘Divas Catwalk’
itakayopambwa na Mama wa Mitindo, Asia Idarous.
Magwji Afua, Mwanahawa, Asya Idarous na Achun Baa meneja wa Gusagusa min Band ndani ya UK.
“Gusagusa
Min Band na Mama wa Mitindo, Asia Idarous, Tayari wapo ndani ya viunga
vya Uingereza na wapo kamili kwa shoo kabambe Mei 2 ndani ya Empire
Suite, London na shoo ya Mei 3, ndani ya Academy, mji wa Northampton.
Gusagusa ipo full band nzima ikijumuisha wapiga vyombo wao” ilieleza
taarifa hiyo kutoka Didas Entertainment.
Aidha,
katika safari hiyo, Asia Idarous ameongozana na wadau wengine wakiwemo
Mkurugenzi wa Gusagusa Mind Band, Hasan Farouk, gwiji wa taarab, Bi Afua
Suleiman (muimbaji), Bi Mwanahawa Ally (muimbaji), Jaffer bhai
(muimbaji), Khamis Chizi (master keyboard ) na Abdulla Ngonda (mpiga
base) na wengineo wengi.
Mama
wa Mitindo, Asya Idarous Khamsin (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi
wa Gusagusa Min Ban, Achun Baa na Hamis chizi 'Master keyboard' ndani ya
viunga vya Milton Keynes UK (Uingereza).
Didas
Entertainment imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za burudani ikiwemo
kupeleka wasanii kutoka Tanzania na kupiga shoo nchini Uingereza pamoja
na shughuli zingjne za Sanaa ikiwemo filamu, wasanii wa filamu na
uandaaji wa filamu, ambapo hadi mwaka huu imeweza kutimiza miaka 10,
tokea kuanzishwa kwake.
Asia Idarous na waimbaji gwiji
Asya Idarous ndani ya pozi kweney viunga vya Milton Keynes United kingdom
Kwa kuweka oda ya kupata tiketi ndani ya UK, whatsapp +447556171941 kwa ku reserve tables.
Asya Idarous na Didas fashions pamoja na Mwanahawa ally
Achuu Baa meneja wa Gusagusa akiwa ndani ya ndege wakati wa kuwasili kwake ndani ya UK tayari kwa shoo hiyo Mei 2 na Mei 3.
No comments:
Post a Comment