Na Magesa Magesa
Octoba, 2024.
Dar es Salaam.
Katika juhudi za kuhakikisha wakulima nchini wanapata maarifa na mafunzo zaidi ya mbinu bora za kilimo.
Kampuni ya EFTA inayojishughulisha na utoajiwa mikopo ya mashine za aina mbalimbali kwawakulima bila dhamana imefadhili wakulimawatano kutoka maeneo mbalimbali nchinikutembelea nchini Uturuki kwa lengo la kujifunza zaidi mbinu bora za kilimo ambazowakulima wa Uturuki wamekuwa wakizitumiakatika kujihakikishia kilimo chenye tija.
Akizungumza kuhusu ziara hiyo MkurugenziMtendaji wa EFTA Bwana Nicomed Bohay, amesema ziara hiyo nimatokeo ya promosheniya “Nunua Trekta Ushinde Safari ya Uturuki"iliyozinduliwa mwezi machi, 2023 ikiwa na lengo la kuwahamasisha wakulima nchinikujitokeza kwa wingi na kukopa Matrekta ainaya New Holland TT75 4WD ambayo kampuniya EFTA iliyanunua kutoka kwa kampuni yaCNH Industrial ya nchini Uturuki ambao ndiowatengenezaji wa Trekta za New Holland Pamoja na zana zingine za kilimo za chapa New Holland.
Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo, Bohay, amebainisha kuwa Lengo kuu la kampeni hiyolilikuwa ni kuhakikisha upatikanaji wa matrektaya New Holland TT75 4WD yanapatikana kwaurahisi nchini pindi wakulima wanapoyahitaji.
“Miaka ya nyuma ilimuhitaji mkulima kusubirisiku sitini hadi tisini kupata Trekta analohitaji ililisafilishwe kutoka uturuki mpaka limfikie, na hii kwa kweli ilikuwa changamoto kubwa sanakwa wakulima wetu na hasa ukizingatia waohutegemea misimu ya mvua kufanya shughuliza kilimo” alisema Bohay
Kwa kuuona ukubwa wa changamoto hiyo kampuni yetu iliamua kununua Trekta zaidi ya200 aina ya New Holland TT75 4WD na kuzileta hapa nchini ili pindi wakulimawanapokuwa wanazihitaji basi waweze kuzipatandani ya muda mfupi. Aliongeza Bohay
Bohay amesema kuchochea mwitiko wa wakulima kununua au kukopa Trekta hizo kwawingi ambazo zilikuwa zikipatikana kwa urahisinchini ndio maana walikuja na wazo laPromosheni hiyo ambayo Pamoja na malengoyake ya msingi ililenga kuwawezesha wakulimawatakaoibuka washindi kujipatia nafasi yakutembelea Kiwanda cha Matrekta cha New Holland nchini Uturuki Pamoja na kujifunzateknolojia mbalimbali ambazo wakulima wa Uturuki huzitumia kujipatia mazao mengi zaidi.
Katika kipindi cha siku nne za ziara , wakulimahawa walitembelea kiwanda cha utengenezajiwa Matrekta cha New Holland nchini Uturuki, ambapo waliona mchakato wa kutengenezamatrekta ambayo kwa sehemu kubwa hutumiwana wakulima wa Tanzania. Ziara hii iliwapauelewa wa kina kuhusu teknolojia na uhandisiunaohusika katika kuunda Matrekta hayoPamoja na mashine zingine.
Ziara hiyo pia ilihusisha warsha na semina, ambapo wakulima walijifunza ubunifumbalimbali katika kilimo endelevu, kilimo hai, na matumizi ya zana za kidijitali katika kilimocha kisasa.
Kwa upande wake kiongozi wa msafara huo, Bw. Clerius Asiel, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Masoko wa EFTA, amesema safari hiyo imekuwa ni fursa muhimu sana kwa wakulimaalioambatana nao kujifunza zaidi mbinu bora za kilimo
“Wakulima hawa tayari wanatumia mbinu za kisasa za kilimo, lakini kutokana na maendeleoya haraka ya teknolojia, kuna mengi zaidi yakujifunza. Ziara hii imewaruhusu kufikiria njeya mbinu walizokuwa wakitumia na kuchunguza jinsi wanavyoweza kutumia mbinuza kisasa zaidi ili kuongeza mavuno yao.”Amesema Clerius
Kwa upande wao baadhi ya washindi wa ziarahiyo wameishukuru sana kampuni ya EFTA kwafursa hiyo ya ziara ya mafunzo nchini Uturukimaana wamejifunza mengi ambayo wameahidikuyatumia katika kuleta mapinduzi katikashughuli zao za kila siku za kilimo.
Peter Keppa ni mmoja wa Washindi wa ziarahiyo akitokea wilaya ya Hanang mkoa wa Manyara, anasema ziara hiyo imemtoa“tongotongo” “ Mwanzoni nilijua kwa kumilikitu Trekta basi tayari unakuwa mkulima wa kisasa, ila ukweli sikuwa sahihi baada ya ziarahii na maarifa niliyoyapata na huku kwawenzetu sasa ndio naenda kuwa mkulima wa kisasa maana nimekusudia elimu yote niliyoipata huku kuitumia kwa usahihi” Amesema Keppa
Kupitia ziara hiyo Keppa amesema wakulimawa Uturuki hawategemei mvua kupata mavuno, “sehemu kubwa ya kilimo chao ni cha umwagiliaji, nadhani huku ndiko hata sisiwakulima wa Tanzania Tunatakiwa tuelekezemawazo yetu sasa, wenzetu mvua siochangamoto kwao, kwa sababu wamewekezasana katika mifumo ya umwagiliaji, ambayoinahakikisha mavuno yao yapo salama muda wote.”
Kwa upande wake Bwana, Nobert Alexander mshindi mwingine aliyepata Bahati ya kuwa kushinda fursa ya kuwa katika ziara hiyo amewashukuru sana kampuni ya EFTA na kuelezea furaha yake kwa maarifa aliyoyapatakatika ziara hiyo.
“Ziara hii imetupa maarifa ambayo hatukuwanayo kabla. Tumeona jinsi teknolojia ya kisasainaweza kurahisisha kilimo, na ninatarajiakutumia yale niliyoyajifunza ili kuongezamavuno yangu, lakini pia nitawashirikisha pia na wakulima wenzangu ili sote kwa Pamoja tufanikiwe.” Amesema Nobert
Mkulima mwingine, Bw. Charles Gidamoni, aliongeza, “Hii ilikuwa ni uzoefu wa kubadilisha maisha. Ujuzi tuliopewahautabadilisha tu mashamba yetu, bali pia utakuwa mwongozo kwa wakulima wenginekatika jamii zetu.”
Kupitia ziara hii wakulima hawa sasa wanaouhakika wa kuboresha kilimo chao kwa kutumiateknolojia mbalimbali za kilimo huku wakiwana uhakika wa kupata mikopo ya mashine za kilimo watakazo zihitaji ili kutoka EFTA biladhamana ili kuongeza ufanisi katika kilimochao.
****MWISHO*****
Washindi wa Nunua Trekta Ushinde Safari YaUturuki wakiwa katika Uwanja wa ndege wa Istanibul mara baada ya kuwasili nchini Uturukitayari wa ziara ya Mafunzo ya Kilimo.
Tazama picha za matukio mbalimbali wakati wa ziarahiyo.
No comments:
Post a Comment