MATUKIO YA KUTISHA: SHEIKH AMWAGIWA TINDIKALI, JIJINI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


1 Mar 2014

MATUKIO YA KUTISHA: SHEIKH AMWAGIWA TINDIKALI, JIJINI ARUSHA

Arusha. Sheikh wa Msikiti Mkuu wa Bondeni jijini Arusha, Mustaph Mohamed Kihago (49) na mtoto wake, Halidi Mustapha (10), wamelazwa Hospitali ya Mkoa Mount Meru kwa matibabu, baada ya kumwagiwa kimiminika kinachodhaniwa kuwa ni tindikali na kuwajeruhi shingoni na usoni.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya wodi ya watoto kwenye hospitali hiyo juzi, Kihago alisema kuwa walimwagiwa tindikali hiyo jana saa 11.10 alfajiri, akiwa anashuka ngazi kwenda kuongoza swala ya alfajiri.
Alisema akiwa eneo la msikiti baada ya kumaliza ngazi ili aingie ndani, alimwona kijana kwa nyuma yake ameshika kopo lenye maji mekundu na ghafla alimmwagia usoni na mengine yalimpata mtoto wake.
Kihago alisema baada ya mtu huyo kumwagia kimiminika hicho, alikimbia. “Baada ya tukio hilo niliingia ndani na mtoto alishindwa kufumbua macho, na mimi nilipata majeraha shingoni,” alisema.
Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP, Japhet Lusingu alisema tukio lilitokea Februari 28 saa 11.15 alfajiri eneo la Msikiti Mkuu wa Bondeni wakati mtu asiyejulikana alipommwamwagia kitu kinachodhaniwa tindikali usoni baba na mtoto wake wakati wakijiandaa kuswali. Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad