Arusha. Sheikh wa Msikiti Mkuu wa Bondeni jijini Arusha, Mustaph
Mohamed Kihago (49) na mtoto wake, Halidi Mustapha (10), wamelazwa
Hospitali ya Mkoa Mount Meru kwa matibabu, baada ya kumwagiwa kimiminika
kinachodhaniwa kuwa ni tindikali na kuwajeruhi shingoni na usoni.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya wodi ya
watoto kwenye hospitali hiyo juzi, Kihago alisema kuwa walimwagiwa
tindikali hiyo jana saa 11.10 alfajiri, akiwa anashuka ngazi kwenda
kuongoza swala ya alfajiri.
Alisema akiwa eneo la msikiti baada ya kumaliza
ngazi ili aingie ndani, alimwona kijana kwa nyuma yake ameshika kopo
lenye maji mekundu na ghafla alimmwagia usoni na mengine yalimpata mtoto
wake.
Kihago alisema baada ya mtu huyo kumwagia
kimiminika hicho, alikimbia. “Baada ya tukio hilo niliingia ndani na
mtoto alishindwa kufumbua macho, na mimi nilipata majeraha shingoni,”
alisema.
Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Kamishna
Msaidizi wa Polisi, ACP, Japhet Lusingu alisema tukio lilitokea Februari
28 saa 11.15 alfajiri eneo la Msikiti Mkuu wa Bondeni wakati mtu
asiyejulikana alipommwamwagia kitu kinachodhaniwa tindikali usoni baba
na mtoto wake wakati wakijiandaa kuswali. Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment