MWANAHARAKATI GIDABUDAY AMKALIA KOONI MTAKA :Mtaka acha ‘utata’ Nyambui siyo pekee anayetambuliwa na IAAF - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


28 Feb 2014

MWANAHARAKATI GIDABUDAY AMKALIA KOONI MTAKA :Mtaka acha ‘utata’ Nyambui siyo pekee anayetambuliwa na IAAF

Anthony Mtaka:Picha na Maktaba



Anthony Mtaka ni mtu ‘mtata’ hafahamu lolote kuhusu riadha, kijana huyo mdogo aliyezaliwa mwanzoni kabisa ya miaka ya 1980 hajui mambo anayoyazungumza katika vyombo vya habari.

Akinukuliwa na ITV juzi jamaa huyo mpenda madaraka alisema “Suleiman Nyambui ndiyo pekee kocha anayetambuliwa na shirikisho la riadha duniani” Hatumlaumu yeye kwa kutojua lolote maana kiongozi huyo mtata hata mashindano ya chekechea hajawahi kukimbia.
Mwalimu Samwel Tupa alipata cheti cha utambuzi wa IAAF tarehe 7/7/1988 wakati yeye akiwa na chini ya umri wa miaka  kumi; hivyo siyo halali yeye kujazwa uongo na ndugu yake wa ukoo (Suleman Nyambui) kwamba yeye pekee ni mtaalamu! Kumbuka SHERIA # 12 ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliivunja ili ukoo wao uongoze riadha. ' Wasikae 'relaxed' eti tutasahau ama tutatulia'
Kwa kauli yake inamaana hata Filbert Bayi, Samwel Tupa na wengine wengi hawana utambuzi wa International Association of Athletics Federation! Kama yeye hana cheti cha IAAF asiwasemee wengine maana huo ni upotoshaji.

Kama alikosea basi arekebisha kauli na ajitahidi kujifunza historia ya riadha ya Tanzania na ya dunia asipotoshe ukweli wa kujinadi katika vyombo vya habari akieleza uongo mtupu. CHANZO :www.gidabuday.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad