Siasa : Madiwani wa Arusha Wakataa Kugawa Jimbo la Arusha Mjini - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 25 March 2025

demo-image

Siasa : Madiwani wa Arusha Wakataa Kugawa Jimbo la Arusha Mjini

WhatsApp%20Image%202025-03-25%20at%2017.38.00%20(1)
WhatsApp%20Image%202025-03-25%20at%2017.38.01

WhatsApp%20Image%202025-03-25%20at%2017.38.00

WhatsApp%20Image%202025-03-25%20at%2017.38.00%20(1)


Na Pamela Mollel, Arusha.


Hatimaye Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Arusha wakubaliana kwa pamoja kutougawa jimbo la Arusha mjini mara mbili,badala yake wamekubaliana kugawanywa kwa kata nane za jiji hilo 


Taarifaa hizi zinakuja wakati mwafaka kuelekea uchaguzi mkuu ambapo hivi karibu zimekuwepo kwa taarifa zisizorasmi zikidai jimbo hili kugawanywa mara mbili kutoka na ukubwa wake


Leo Machi 25 ,2025 Madiwani wamevunja ukimya kwa kukataa kwa pamoja madai ya kuugawa jimbo Arusha kwa madai kuwa halina ukubwa wa kutisha katika kuwahudumia wananchi 


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha,mara baada ya kumalizika kwa baraza maalum la Madiwani,Meya wa jiji Maxmillian Iranqhe anasema kuwa walichokubaliana katika kikao hicho ni kugawanywa kwa kata nane tu,ambazo zimeonekana kuna changamoto katika kuwafikia wananchi na kushindwa kutatua kero kwa wakati kutokana na ukubwa wa eneo


"Mpaka sasahivi tulichokubaliana zigawanywe kata hizo nane na tumefanya hivyo ili kuharakisha maendeleo katika kata husika ili kuweza kutatua kero kwa wananchi "Anasema Iranqhe 


Aidha ameongeza kuwa Madiwani wamepitisha kata ya Muriet,Moshono,Sokoni1,Sinoni,Lemara na Terat


Kwa upande wake diwani wa kata ya Sakina Vicent Willson anasema kugawanywa kwa kata hizo ni mapendekezo kutoka kwa baadhi ya madiwani wa kata hizo ambazo zinaonyesha changamoto wanazokutana nazo katika kuwahudumia wananchi kutokana na ukubwa wa eneo 


"Jimbo la Arusha lina ukubwa wa kilometa za mraba 272 hatujaona sababu za msingi za kuugawa ila kwenye kata ni Sawa maana kuna kata zingine ni kubwa sana inabidi utembee umbali mrefu katika kuwahudumia wananchi"Anasema Willson


WhatsApp%20Image%202025-03-25%20at%2017.38.00%20(1)


No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *