Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa kufungua semina ya 'Research Workshop' yenye lengo la kutoa mafunzo maalumu ya kuwandaa wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti kabla ya kuhitimu mafunzo kutoka bodi hiyo yanayofanyika katika ukumbi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Amani Ngonyani akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa semina ya 'Research Workshop' yenye lengo la kutoa mafunzo maalumu ya kuwandaa wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti kabla ya kuhitimu mafunzo kutoka bodi hiyo yanayofanyika katika ukumbi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi alipokuwa anafungua mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku tano katika ukumbi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti waliofika kwenye semina iliyoandaliwa na Bodi hiyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jijini Dar es Salaam.
BODI ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeandaa Semina ya 'Research Workshop' na kutoa mafunzo maalumu ya kuwandaa wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti kabla ya kuhitimu mafunzo kutoka bodi hiyo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Godfrey Mbanyi amesema kuwa moja ya matakwa ya CPSP ni kufanya 'Research Paper' na mwanzo wake ni huo kwa wanafunzi kuhudhuria semina na kupata mafunzo yatakayowapitisha kwa usahihi katika safari yao ya kufanya tafiti na kuhitimu vyema mafunzo hayo kwa mujibu wa bodi hiyo.
Mbanyi amesema, katika mafunzo hayo wanafunzi watapitishwa katika maeneo tofauti tofauti ya mbinu za utafiti na andiko la utafiti pamoja na kuwajengea uwezo wa kuandika tafiti na ripoti mbalimbali kwa kufuata kanuni na miongozo ya PSPTB katika tafiti zao watakazozifanya ikiwemo na kuzitetea Tafiti hizo.
Aidha amesema kupitia mafunzo hayo wanafunzi wataelekezwa na kujengewa uwezo wa jinsi ya kuandaa andiko la utafiti hususani ya PSPTB ili waweze kuhitimu mafunzo hayo na kuwataka wanafunzi hao kuzingatia umuhimu wa mafunzo hayo muhimu katika tafiti zao watakazozianza mara baada ya mafunzo hayo.
Mafunzo hayo ya siku 5 yaliyoanza leo Agosti 12 hadi Agosti 16, 2024 yamewakutanisha wanafunzi zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo Kilimanjaro, Mtwara, Mwanza na wenyeji Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment