Habari : Rais Samia Akabidhi cheti cha Pongezi TANAPA kwenye Tamasha la Kizimkazi Festival 2024 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 25 August 2024

Habari : Rais Samia Akabidhi cheti cha Pongezi TANAPA kwenye Tamasha la Kizimkazi Festival 2024




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan amekabidhi cheti cha pongezi kwa ushiriki wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwenye tamasha la Kizimkazi Festival 2024 Hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu ndogo Kizimkazi Zanzibar.

Cheti hicho cha pongezi kimepokelewa kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Nassoro Juma Kuji, na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Jully Bede Lyimo - Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara pamoja na Afisa Uhifadhi Mwandamizi Amina R. Salum ambaye ni Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa Ruaha.

TANAPA, kwa dhati na unyenyekevu mkubwa tumepokea na kuthamini heshima hii kubwa kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment