Habari : Monduli Yafanikiwa Kufikia 22.77% ya Usasishaji Anuani za Makazi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 23 August 2024

demo-image

Habari : Monduli Yafanikiwa Kufikia 22.77% ya Usasishaji Anuani za Makazi


IMG-20240822-WA0008Na Mwandishi Wetu.

Wakati zoezi la uhakiki, usasishaji na usajili wa Anwani za Makazi likiendelea katika Halmashauri sita za Mkoa wa Arusha, Halmashauri ya Monduli imefanikiwa kufikia asilimia 22.77 ya usasishaji anwani za makazi ndani ya siku 5 kutoka Agosti 17 hadi  21 mwaka huu 2024.

Akizungumzia maendeleo ya zoezi hilo ofisini kwake tarehe 21  Agosti, 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Bi Happiness Laizer, amesema Anwani zilizosasishwa hadi leo mchana ni  6621 kati ya 29,082 zilizosajiliwa mwaka 2022.

Bi. Laizer amesema anwani mpya zilizosajiliwa ni 1,358 sawa na ongezeko la asilimia 4.67 yakiwa ni mafanikio makubwa kwa eneo hilo linalokaliwa na jamii ya Kimasai.

IMG-20240822-WA0010
IMG-20240822-WA0009
Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa walipotembelea Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness Laizer, tarehe 21 Agosti, 2024.

Pamoja na mambo mengine wamezungumzia zoezi la Uhakiki, Usasishaji wa Anwani za Makazi na Usajili wa Anwani mpya linaloendelea pamoja na matumizi ya Mfumo wa programu Tumizi ya NaPA na huduma ya Barua ya Utambulisho Kidigitali.

IMG-20240822-WA0017
IMG-20240822-WA0016
IMG-20240822-WA0015
Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa walipotembelea Kaburi la Hayati Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu katika Serikali ya Awamu ya Nne lililopo nyumbani kwake Kijiji cha Ngarashi, Halmashauri ya Wilaya ya Monduli. 

Timu hiyo ya wataalamu ikifika katika makazi ya kiongozi huyo wakati wa zoezi la Uhakiki wa Anwani za Makazi linaloendelea katika kijiji hicho tarehe 21 Agosti, 2024.
IMG-20240822-WA0014
IMG-20240822-WA0013
Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa walipotembelea makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Moringe Sokoine yaliyopo katika Kata ya Monduli Juu, Halmashauri ya Wilaya ya Monduli. 

Wataalam hao walipata nafasi hiyo wakati wakikagua maendeleo ya zoezi la Uhakiki wa Anwani za Makazi ambapo walipata nafasi ya kutembelea Kaburi la Kiongozi huyo lililopo nyumbani kwake tarehe 21 Agosti, 2024.

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *