Habari : KIKWETE akutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa ATE Jijini Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 16 August 2024

Habari : KIKWETE akutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa ATE Jijini Dodoma

Na Jane Edward


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo m na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi. Ndomba Doran.

Katika mazungumzo hayo walijadili kuhusu masuala mbalimbali ya waajiri hapa nchini pamoja na kuona namna ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kutatua changamoto zinazo ikabili sekta hiyo.

Awali wakati wa kumkaribisha Waziri Kikwete Bi Ndomba aliongozana na Meneja wa Kanda ya Kati wa ATE, Bw. Leonard Mapha alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.

Hata hivyo kukutana huko ni muendelezo wa ziara ya Waziri huyo kujitambulisha katika maeneo yaliyo chini ya wizara yake baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.



No comments:

Post a Comment