Jamii : Elimu Itolewe kwenye ushiriki wa kutoa maoni katika ngazi ya Uamuzi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

18 Jul 2024

Jamii : Elimu Itolewe kwenye ushiriki wa kutoa maoni katika ngazi ya Uamuzi

WADAU wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS),wameshauri utoaji wa kwenye elimu jamii kuhusiana na umuhimu wa ushiriki wa kila mtu kwenye kutoa maoni katika ngazi za maamuzi kuanzia nyumbani hadi kufikia kwenye serikali kuu.


Akizungumza Julai 17,2024 Jijjini Dar es salaam,katika viunga vya ofisi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Mwanaharakati wa masuala ya Jinsia, Silivia Sostenes amesema jamii inatakiwa ielewe umuhimu wa ushiriki katika mgawanyo wa mali na rasilimali kuanzia ngazi ya familia kabla ya kufikia katika ngazi ya Taifa.

Aidha Slivia ameeleza kuwa wametambua muhimu kwa kila mtu kutoa maoni yake hasa kwenye vikao vinavyoanzia katika ngazi ya mtaa hadi ngazi za juu.

"Kuna umuhimu mkubwa kwa kila mmoja kuchangia mawazo yake kwenye uongozi,kukosoa na kupongeza pale inapotakiwa" Slivia ameeleza.

Pamoja na hayo Silvia amegusia suala la mgawanyo sawa wa mali na rasilimali ambapo amesema ni muhimu kila kundi likahusishwa bila kuacha kundi lolote kuanzia ngazi za chini kabisa kwenye familia hadi serikali kuu.

Kwa upande wake, Mwanaharakati wa Jinsia Cesilia Michael ameiomba serikali kuhusisha wananchi katika mipango yao kwa lengo la kuhakikisha huduma wanazozitoa zinakidhi mahitaji jamii.

Nae, Mdau wa Semina za Jinsia kata ya Manzese, Wilaya ya Ubungo, Kennedy Anjelita amesema rasilimali zinazotengwa na serikali haziwanufaishi walengwa moja kwa moja kutokana na uongozi kuwanufaisha watu wao wa karibu.

"Serikali lengo lao kila mtu anufaike lakini mchakato wa maandalizi hadi kufikia hatua ya mwisho hauko sawa,kutokana na baadhi ya viongozi ambao wanasimamia hizo rasilimali kutokuwa na usawa wakijinsia"amesema.






No comments:

Post a Comment


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633