Uchumi: Waziri Dkt. Mwigulu kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa SADC - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


11 Jul 2021

Uchumi: Waziri Dkt. Mwigulu kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa SADC


DAR ES SALAAM:Tarehe 12 Julai, 2021:Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Mawaziri wanaohusika na masuala ya Fedha na Uwekezaji wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jopo la Mapitio ya Uchumi Mpana (Peer Review Panel).

Mkutano huo utafanyika chini ya Mwenyekiti Waziri wa Uchumi na Fedha wa Msumbiji Mhe. Adriano Afonso Maleianetarehe 15 Julai, 2021 kwa njia ya mtandao kutokea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es salaam, ambapo utatanguliwa na kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, Uwekezaji na Maafisa Waandamizi wa Benki Kuu za SADC, utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 12-13 Julai, 2020.

Mkutano huo utawakutanisha Mawaziri wenye dhamana na masuala ya Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi 16 wanachama wa SADC na utajadili masuala ya Fedha na Uwekezaji pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji katika mkutano uliofanyika mwezi Julai 2020Dar es SalaamTanzania.

Vilevile mkutano huo utajadili kwa kina na kutoa maamuzi ya kisera kuhusu athari za Kiuchumi na Kijamii za COVID-19 pamoja na mambo mengine kadhaa.

Imetolewa na

Benny Mwaipaja

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad