Burudani : Fomu za Miss Tanga 2021 kuanza kutolewa Agosti 1 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 11 July 2021

Burudani : Fomu za Miss Tanga 2021 kuanza kutolewa Agosti 1

 

Muandaaji wa Shindano la Miss Tanga 2021  kupitia Kampuni yake ya Chuchu Double Touch Entertainment Chuchu Hans akizungumza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Tanga kuhusu kushoto ni Wilson Untouchable ambaye ni mmoja wa wanakamati wa mashindano kulia ni Mwalimu ambaye atakuwa akiwanoa walimbwende hao Pili Miraji
Muandaaji wa Shindano la Miss Tanga 2021  kupitia Kampuni yake ya Chuchu Double Touch Entertainment Chuchu Hans akizungumza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Tanga kuhusu kushoto ni Wilson Untouchable ambaye ni mmoja wa wanakamati wa mashindano kulia ni Mwalimu ambaye atakuwa akiwanoa walimbwende hao Pili Miraji
Wilson Untouchable ambaye ni mmoja wa wanakamati wa mashindano akizungumza jambo wakati wa mkutano huo kulia ni Muandaaji wa Shindano la Miss Tanga 2021  kupitia Kampuni yake ya Chuchu Double Touch Entertainment Chuchu Hans akifuatiwa na Mwalimu ambaye atakuwa akiwanoa walimbwende hao Pili Miraji
Mwalimu ambaye atakuwa akiwanoa walimbwende hao Pili Miraji akizungumza jambo wakati wa mkutano huo kushoto ni Muandaaji wa Shindano la Miss Tanga 2021  kupitia Kampuni yake ya Chuchu Double Touch Entertainment Chuchu Hans akifuatiwa na Wilson Untouchable ambaye ni mmoja wa wanakamati wa mashindano hayo
Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakichukua matukio kwenye mkutano huo



SHINDANO la kumsaka Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2021) limeiva baada ya kamati inayoandaa mashindano hayo kutangaza kwamba Agosti 1 mwaka huu fomu za usaili zitaanza kutolewa kwa washiriki.

Hayo yalibainishwa leo na Muandaaji wa Mashindano hayo kupitia Kampuni yake ya Chuchu Double Touch Entertainment Chuchu Hans wakati mkutano wake na wandishi wa habari uliofanyika mjini Tanga ambapo alisema maandalizi yote yamekamilika.

Alisema kwamba msimu huu wamejipanga vema kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa na mvuta na ushindani huku akieleza kwamba yatawahusisha zaidi wakazi wa Tanga.

“Hivyo kupitia mkutano huu niwaalike wakazi wa Mkoa huu na wilaya zake na vitongoji kuchangamkia fursa ya kushiriki mashindano haya kwa sababu mashindano ya Urembo ni heshima na kazi”Alisema

Akizungumza namna walivyojipanga kuyafanyia kuwa ya kipekee tofauti na miaka ya nyumba alisema waliandaa Miss Tanga 2019kwa mara ya mwisho kabla ya kuingia Covid 19 na walikua bora katika uandaaji hivyo wataendelea kuboresha zaidi katika shindano la mwaka huu

“Ndugu zangu mjitokeze kwani urembo ni heshima na kama mnavyoona warembo wanapata nafasi mbalimbali za uongozi lakini pia ni ajira hivyo washiriki wajitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa “Alisema

Kwa upande wake Wilson Untouchable ambaye ni mmoja wa wanakamati wa mashindano hayo alisema washiriki wote wanan afasi ya kushinda na wakipata nafasi ya kuingia kwenye mchujo tayari ni mshindi kwa kuwa wote zawadi watapata.

Untouchable alisema ukiachana na washindi watatu,waliobaki watapata fursa za nafasi mbalimbali kupitia wadhamini kwani kuna mdhamini anaweza kumuona mshiriki akawa Balozi wa bidhaa Fulani katika kampuni yake.

Naye kwa upande wake Mwalimu ambaye atakuwa akiwanoa walimbwende hao Pili Miraji aliwataka mabinti wa mkoa huo kuchangamkia fursa ya kushiriki kwenye mashindano hayo .

Alisema kwa kuwa hakuna mshiriki anayepangwa kwa ajili ya kuwa Mshindi amesema hilo kwao halipo na halitatokea katika mkoa wa Tanga.

"Ndugu zangu msiwe na wasiwe wala woga kuhusu mchakato wa Mshindi upo wazina hata Miss Tanzania imebadilika kwa kuwa waandaaji wengi wamekuwa washiriki wa Mashindano ya Ma-Miss kwa miaka ya nyuma,hivyo ubora wa Mshindi ni kutokana na vigezo na kujiandaa kwake kuwaMshindi"alisema Pili.

Pia wameomba wadhamini wajitokeze kwa wingi ili mashindano yaweze kunoga na washiriki waweze kufaidika.

No comments:

Post a Comment