Michezo : Tamisemi na Wabunge Wafanya Mazoezi ,Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


16 Apr 2017

Michezo : Tamisemi na Wabunge Wafanya Mazoezi ,Dodoma









Vikundi vya Jooging kutoka Dodoma vikiwa katika mazoezi ya kukimbia kutoka Viwanja vya Nyerere Square hadi Viwanja vya Kilimani Club Mjini Dodoma.







Vikundi vya Jooging kutoka Dodoma vikiwa katika mazoezi ya viungo katika viwanja vya Kilimani Club Mjini Dodoma.

Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku Bilago(kushoto) Mbunge wa Kiwani (Zanzibar) Mhe. Abdalla Haji Ali (kulia) wakifanya mazoezi ya viungo katika katika viwanja vya Kilimani Club Mjini Dodoma ikiwa ni kuunga mkono wito wa Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan wa kufanya mazoezi.
Mratibu wa Michezo Kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Salum Mkuya akizungumza navikundi vua Jogging Club wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Viwanja vya Kilimani Club Mjini Dodoma.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini Daniel Shija akizungumza na vikundi vua Jogging Dodoma na kuwahakikishia Ulinzi na usalama katika mazoezi yao.

Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku Bilago(kushoto) Mbunge wa Kiwani (Zanzibar) Mhe. Abdalla Haji Ali(katikati) pamoja na Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde(kulia) wakijadiliana jambo na kupongezana mara baada ya kumalizika kwa mazoezi katika viwanja vya Kilimani Mjini Dodoma. Picha/Habari na Raymond Mushumbusi

Ofisi ya Rais TAMISEMI na baadhi ya wabunge wameongoza vikundi vya Jogging Mkoani Dodoma kufanya mazoezi kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Sluhu Hassan wa kufanya mazoezi.

Akizungumza baada ya mazoezi hayo Afisa Tawala kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Rose Lugendo amewaomba wakazi wa Dodoma wajitokeze kwa wingi kufanya mazoezi kwa afya zao na kuimarisha mahusiano baina yao.

“Napenda kuwashauri wakazi wa Dodoma kujiunga na Jogging Clubs na kuwa na Utamaduni wa kufanya mazoezi kwa Afya zao” alisisitiza Bibi Rose.

Kwa upande wake Mbunge Wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde amewaasa vijana kujitokeza kufanya mazoezi kila siku na sio kusubiri kufanya mazoezi mara moja kwa mwezi kwasababu mazoezi ni sehemu ya maisha.

“Vijana tumieni fursa hii kufanya mazoezi na kujenga afya zenu mazoezi yawe sehemu ya maisha yenu” alisisitiza Mhe. Lusinde.

Naye Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku Bilago amevipongeza vikundi vya Jogging Dodoma kwa kuleta mwamko wa mazoezi katika mkoa wao na kujenga desturi ya watu kupenda mazoezi na michezo.

Aidha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini Daniel Shija amewahakikishia ulinzi wanamazoezi na michezo kwa ujumla katika sehemu mbalimblai ambazo watakuwa wanafanya michezo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad