Habari : Waandishi wa Habari za Bunge Wajengewa Uwezo kuhusu Sheria ya Huduma za Habari, Haki na Wajibu wao juu ya sheria hizo. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


6 Feb 2017

Habari : Waandishi wa Habari za Bunge Wajengewa Uwezo kuhusu Sheria ya Huduma za Habari, Haki na Wajibu wao juu ya sheria hizo.


Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakifu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamefanya semina ya siku moja na waandishi wa habari mkoani Dodoma katika ukumbi wa Hazina Ndogo, iliyolenga kuboresha utendaji katika kazi zao.

Mjadala huu umelenga kuwajengea wanahabari uwezowa utendaji wao wa kazi.Waandishi wa habari hao wamejengewa uwezo kuhusu sheria ya huduma zavyombo vya habari ili kuleta ufanisi katika majukumu yao. Mkutano huu umefanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.

Mhariri mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitoa mada kwa wanahabari waliofika kwenye semina iliyokuwa ikihusu utendaji kazi wao wa kila siku.



Wakili wa Mahakama Kuu na Mhariri wa Zamani, James Marenga akitoa mada inayohusisha sheria mbalimbali zinazohusiana na waandishi wa habari na namna ya kufanya kazi bila kuvunja sheria zilizowekwa.

Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo kwenye semina ya Wanahabari uliofanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akizungumza jambo kwenye semina iliyowakutanisha wanahabari mbalimbali waliokutanishwa na Misa Tanzania ili kujadili changamoto zinazowapata katika kazi zaohasa za bungeni.









Baadhi ya waandishi wa habari wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kwa watoa mada waliowasilisha mada mbalimbali katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.











Baadhi ya waandishi wa habari waliofika katika semina iliyoandaliwa na Misa Tanzania kujadili namna ya kufanyakazi kifanisi katika majukumu yao ya kila siku

Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad