Nishati : Waziri , Mwijage Apongezwa kwa Ujenzi wa Kiwanda cha Vigae - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Jan 2017

Nishati : Waziri , Mwijage Apongezwa kwa Ujenzi wa Kiwanda cha Vigae



Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.

Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wa Mwisho Kulia akitoa maelekezo kwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng.

Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng,wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.

Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng (kushoto) wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.

Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng,wakiwa na timu ya ukaguzi wa eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.

Eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. Picha na Othman Michuzi



Na.Mwandishi Wetu
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amepongeza jitihada zinazofanywa na muwekezaji wa kampuni TwyFord Tanzania Cereramics,kwa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae "Tiles" katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.


Waziri Mwijage, amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo, litakalojengwa kiwanda hicho cha kutengeneza vigae "Tiles" kitakachotoa ajira kwa watanzania zaidi ya elfu mbili katika mfumo rasmi,na ajira elfu nne zisizo rasmi.


Waziri Mwijage aliongeza kuwa," bidhaa hizo pia zitauzwa katika nchi majirani kama Zambia,Malawi, DRC,Rwanda, Burundi,Uganda na Jamhuri ya watu wa Afrika Kati na kusafirishwa nje ya bara.


Kwa upande Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho kipo katika hatua ya mwanzo ya Ujenzi na kinataraji kukamilika Mwezi wa Saba na kufunguliwa Rasmi mwezi wa Nane mwaka huu.


Ridhiwani alisema kuwa kiwanda hicho kitasaidia kufungua mji wa Chalinze na kufanya mji wa viwanda na biashara na hivyo kufungua fursa za kiuchumi na kupanua mji huo,katika sekta ya viawanda inayosimamia vyema na serikali ya awamu ya tano.


“ujenzi wa kiwanda hiki ni Alama Chanya ya jinsi serikali ya awamu ya Tano ilivyojidhatiti kufungua fursa za viwanda katika Nchi yetu.Wananchi wa Chalinze na Pwani wameaswa kuendelea kujipanga kwa viwanda na fursa nyingi zaidi.”alisema ridhiwani

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad