Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuwa na tabia ya kuyafanyia muendelezo yale mema wanayoyafanya, kama walivyofanya kampuni ya NIDA TEXTILES kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W).
Akizungumza katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Alhaji Mwinyi amesema kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa akifunga kila siku ya Jumatatu ikiwa ni ishara ya kusherekea siku aliyozaliwa.
Hivyo ni vyema kuiga mfano huo wa kufanya matendo mema kwa kuyarudia mara kwa mara na kuyadumisha, huku akipongeza uongozi wa NIDA kwa kuwaalika na kusherekea pamoja kwani amejifunza mengi kupitia mawaidha yaliyotolewa na viongozi wa dini waliohutubia akiwemo Sheikh Ally Basaleh.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali akiwemo Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Gharib Bilal, Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Naibu Waziri Wizara ya Afya Hamis Kigwangala, Waziri wa zamani wa Ulinzi Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega. Viongozi wa dini waliokuwepo ni pamoja na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Kadhi Mkuu wa Tanzania Abdallah Mnyaa.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali juu ya watanzania kuyafanyia muendelezo wa yale mema kama walivyofanya kampuni ya NIDA TEXTILES kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W). leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali katika kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W). leo jijini Dar es Salaam.
Shehe Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Sheikh Alhadi Mussa Salim akizungumza machache katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dk. Hamisi Kigwangalla leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waumini wakiwa katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waumini wakiwa katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waumini wakiwasili katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba kwenye hafla hiyo
Sehemu ya viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo, Al-Haji Ali Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuwa na tabia ya kuyafanyia muendelezo yale mema wanayoyafanya, kama walivyofanya kampuni hiyo ya Nida na kuwakutanisha pamoja waislamu na kumsifu katika kumbukumbu hizo za kiongozi wa waislamu Mtume Muhammad (S.A.W).
Tazama MO tv kuona tukio hilo hapa:
Mbali na Dk. Kigwangalla, wageni wengine ni pamoja na Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Waziri wa zamani wa Ulinzi Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega huku kwa viongozi wa dini walikuwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Kadhi Mkuu wa Tanzania Abdallah Mnyaa ambapo wote kwa pamoja walipewa zawadi maalum na kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya maulidi ya Mtume
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali katika tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijadiliana jambo na wageni waalikwa wengine katika tukio hilo akiwemo Prof. Ibrahim Lipumba
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni katika hafla hiyo ya maulidi ya Mtume
Baadhi ya vijana wa Madrasa mbalimbali kutoka Dar es Salaam na baadhi ya mikoa wakifuatiliatukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Naibu waziri wa Tamisemi, Mh. Suleiman Jafo wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya maulidi ya Mtume
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijadiliana jambo na Naibu waziri wa Tamisemi wakati wakiwasubiria wageni waalikwa akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakati wa kumpokea alipowasili kwenye hafla hiyo.
dua zikiendelea
Dua zikiendelea
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi, akizungumza katika tukio hilo
Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipokea zawadi kwenye hafla hiyo.
Dk. Kigwangalla akipokea zawadi katika hafla hiyo
Wageni mbalimbali wakifuatilia hafla hiyo ya Maulidi
No comments:
Post a Comment