Matukio : DC Awaagiza wakuu wa shule za sekondari kuwa na kiwango cha ufaulu kuanzia asilimia 41 - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


22 Sep 2016

Matukio : DC Awaagiza wakuu wa shule za sekondari kuwa na kiwango cha ufaulu kuanzia asilimia 41


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Wakuu wa Shule za sekondari Wilayani humoBaadhi ya walimu wakisikiliza kwa makini maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi

Na Mathias Canal, Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi amewaagiza wakuu wa shule za Sekondari zote za Wilaya hiyo kuhakikisha wanafikia ufaulu kuanzia asilimia 41% ili kuakisi hali ya ukuaji wa ufaulu nchini na kupata wanafunzi waliopikwa vyema darasani ili kuwa na wasomi wenye weledi pasina mashaka.

Dc Ndejembi amesema kuwa hatarajii kusikia shule mojawapo Wilayani humo ikiwa imeshika mkia Kiwilaya, Mkoa ana Taifa kwani kufanya hivyo ni kuonyesha jinsi ambavyo walimu hawakujiandaa vyema katika kuwaimarisha wanafunzi darasani ili kufikia ufaulu mahususi na kulijenga Taifa letu katika misingi bora ya elimu.

Ndejembi alisema kuwa anataraji kushirikiana na Afisa elimu sekondari ili kutoa hamasa kwa shule ambazo zitafanya vyema katika mitihani yao ili kuamsha ari kwa shule zingine Wilayani humo.
Walimu hao wametakiwa kutofanya kazi kwa mazoea, kuwa na hofu ya Mungu, na kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa katika kufundisha wanafunzi kwani walimu wana wajibu mkubwa wa kuwafanya wanafunzi kufaulu katika mitihani yao.

Sambamba na hayo pia Dc Ndejembi amewataka walimu hao kutokuwa na madaraja kati yao na wanafunzi wao kwani kufanya hivyo ni kutengeneza chuki kutoka kwa wanafunzi kwenda kwa walimu ambapo pia inapelekea kuyachukia masomo yanayofundishwa na walimu hao.

Post Top Ad