Golikipa wa Ndanda FC, Jeremiah Kisubi akiokoa moja ya hatari langoni mwake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Yanga. Yanga imeshinda 4-0. (Picha na Francis Dande).
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akimtoka beki wa Ndanda FC, Nassoro Kapama katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Yanga ilishinda 4-0.
Wachezaji Juma Abdul, Vicent Bosoou na Simon Msuva wakishangilia bao la 4 la timu hiyo lililofunga na Bossou.
Beki wa Yanga, Vicent Bossou akipiga kichwa mpira uliozaa bao la 4 la timu hiyo wakati ilipopambana na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Uhuru.
Bossou akikumbatiana kwa furaha na Juma Abdul baada ya kuipatia Yanga bao la 4.
No comments:
Post a Comment