Matukio : Rais Dk. Magufuli awaapisha viongozi mbalimbali ,Ikulu Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 10 December 2016

Matukio : Rais Dk. Magufuli awaapisha viongozi mbalimbali ,Ikulu Jijini Dar es Salaam



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Christopher Olonyokie Ole -Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Grace Alfred Martin kuwa Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya mambo ya Nje Ikulu jijini Dar es Salaam.

Viongozi walioapishwa wakila kiapo cha Maadili mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Alfred Martin, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe pamoja na Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole-Sendeka.

Viongozi walioapishwa waki weka saini katika viapo vya maadili Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Alfred Martin, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na utalii Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe pamoja na Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole Sendeka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na viongozi walioapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe, Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole Sendeka, Wakwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Alfred Martin pamoja na Katibu Mkuu wa Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.