Zanzibar : Sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa mtume Muhammad (SAW), Unguja - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


13 Dec 2016

Zanzibar : Sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa mtume Muhammad (SAW), Unguja



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Sheikh Sherali Champsi mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,

Baadhi ya Viongozi na waalikwa mbali mbali wakiwa katika Sherehe ya kuadhimisha Maulid ya kuzalia Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na wake wa Viongozi mbali mbali na Wananchi wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya Maulid ya kuzalia Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein

Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) katika Maulid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuangalia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akitia ubani kama ishara ya Kuyafungua Maluid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Waislamu na Wananchi waliohudhuria katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Ustadh Ali Muombwa Hassan wa Chuo cha Kiislamu akitoa Tafsiri ya Qur'aan Tukufu ya Suratul Touba (Aya 128 hadi 129) iliyosomwa katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Wanafunzi wa Madrassa Hidayatul Munineema na Nurul Islamia ya Mpendae Mjini Unguja wakisoma Qaswida YaRabii Swali katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Ustadh Mohamed Khamis Rashid wa Kiweani Pemba akisoma maulid Barzanji mlango wa kwanza katika sherehe tukufu ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akifukiziwa Udi baada bya kutiliwa marashi wakati kumswalia mtume Muhamad (S.A.W) wakati sherehe ya maadhimisho ya maulid

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mw3anamwema Shein (katikati) pamoja na Wake wa Viongozi wakisimama kumswalia Mtume (S.A.W) wakati wa Maulid hayo.

Mashekhe mbali mbali na wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa Kiongozi wetu Mtume Muhammad (S.A.W) wakisimama kumswalia jana katika sherehe zilizofanyika katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipookea Zawadi ya Qaswida ya mwaka kutoka kwa Sheikh Sherali Champsi, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) wakati wa sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Sheikh Mohamed Kassim akitoa Khutba yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Wanamadrssa kutoka Mtendeni Mjini Unguja wakisoma Maulid ya Hom wakati wa sherehe za maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)

Akina mama waliojitokeza katika sherehe za maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)

Wanafunzi wa Madrassa mbali mbali na Wananchi wakiwa katika sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Sheikh Sherali Champsi Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) baada ya kumalizika kwa sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,(kushoto) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.Picha na IKULU, Zanzibar

Post Top Ad