Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa
Mataifa litakalotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya
Umoja wa Mataifa
Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya
mji wa
Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Mahakama hiyo wakati
ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa litakalotumika kutunza
kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa
Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya
mji wa
Arusha, kutoka kushoto ni John Hocking (Msajili MICT ), Theodor Meron
(Rais wa MICT ) , Miguel de Serpa Suares (Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Taifa katika masuala ya kisheria ) ,kulia ni Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Mkuu wa mkoa wa Arusha mhe.
Mrisho Gambo,Serge Brammertz (Mwendesha Mashitaka wa MICT ) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia)
.......................................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amezindua majengo ya ofisi za Umoja wa Mataifa
zitakazotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa
Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa
Arusha.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua
majengo hayo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta
John Pombe Magufuli na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kudumisha mahusiano
Majengo hayo yamejengwa katika eneo la Laki
laki mkoani Arusha baada ya Serikali ya Tanzania kuipatia Umoja wa
Mataifa eneo lenye ukubwa wa ekari 16.17 bure kwa ajili ya kujenga hayo
ya kihistoria hapa nchini.
Tanzania
inaomba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kusaidia kupatikana kwa
wote waliohusika na mauaji hayo ya kimbari ili kuhakikisha haki
inapatikana kwa wahanga wa mauaji hayo.