Mafundi wakijenga eneo lilipotua Bomu kama kumbukumbu ya kudumu iliyopoteza maisha ya watu na kujeruhi.
Na Filbert Rweyemamu -Arusha
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini,Fransisco Padilla
anatarajiwa kuzindua Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi
Olasiti leo ambalo lilikua lizinduliwe May 5 mwaka baada ya kutokea shambulio la
bomu la kutupwa kwa mkono.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo amewataka waumini na wananchi
kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kanisani hapo kwani
ulinzi umeimarishwa kuhakikisha jambo hilo
linafanikiwa.
Alisema mbali ya Balozi wa Papa watakuwepo maaskofu wote kutoka
baraza la maaskofu katoliki nchini(Tec)viongozi mbalimbali wa taasisi na
serikali.
Kwa upande Mwenyekiti wa Parokia hiyo,Julius Mbaga alisema
maandalizi ya uzinduzi yamekamilika na waumini wamejiandaa kiroho na kimwili
katika siku hiyo muhimu.
“Tunatarajia wageni watu wasiopungua 3,000 na mambo matatu
yatafanyika kwa wakati mmoja,Balozi Padilla atafungua kanisa letu na Askofu Mkuu
wa Jimbo Kuu la Arusha,Josephat Lebulu atatabaruku na kuweka wakfu nyumba za
madri,”alisema Mbaga
May 5,mwaka huu wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo lilifanyika
shambulio la kigaidi lililosababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa
vibaya na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi wahusika kusakwa popote
walipo.
|
No comments:
Post a Comment