Na Chalila Kibuda.
NAIBU
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amewaasa abiria kutoa
taarifa pale wanapoona dereva anahatarisha maisha yao katika vyombo vya
usafiri.
Masauni
ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti
iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo
cha mabasi ya Mikoani na Nchi Jirani cha ubungo jijini Dar es Salaam,
amesema kila mtu anawajibu wa kutoa taarifa dhidi ya dereva
anayehatarisha maisha katika vyombo vya usafiri.
Amesema
dereva kutojua sheria za usalama barabarani isiwe kigezo cha kuvunja
sheria zilizowekwa kutokana na waathirika wa ajali ni watanzania ambao
ndio nguvu kazi ya taifa.
Amesema
kampeni hiyo iweze kuleta matokeo chanya ambayo yataonyesha kupungua
kwa ajali au kutokuwepo kwa ajali na kufanya watanzania kuwa salama
katika vyombo vya usafiri.
Nae
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishina wa
Jeshi la Polisi (DCP), Mohamed Mpinga amesema kampeni iliyozinduliwa ni
jitihada za kikosi cha usalama barabarani katika kupambana na ajali
pamoja na kuongeza askari kila sehemu ambayo dereva wamekuwa wakikiuka
sheria za usalama barabarani.
Amesema
abiria wanatakiwa kuwa chachu ya kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za
usalama barabarani kwa madereva ili waweze kuchukulia hatua.
Mjumbe Usalama barabarani Mkoa Dar es Salaam, Idd Azzan amesema kampeni hiyo ni italeta mageuzi katika kupunguza ajali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kushoto) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti
ndani ya basi la Machame Express katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini
Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo iliandaliwa na Mabalozi wa RSA kwa
kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza na abiria mara baada ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti
katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka
abiria nchini kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona dereva anavunja sheria na
pia kila abiria ni wajibu wake kujua haki zake. Kushoto ni Mlezi wa RSA Taifa
ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna,
Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kulia) akimsikiliza Katibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) Taifa,
Asina Omary alipokuwa anatoa historia ya RSA pamoja na majukumu yake kabla
ya Naibu Waziri huyo kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti katika Kituo Kikuu
cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo iliratibiwa na
Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kushoto) akienda kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti na Mabalozi wa
Usalama Barabarani nchini (RSA) ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini
Dar es Salaam. Masauni alizindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyoratibiwa na
Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini. Watatu kushoto
ni Mlezi wa RSA Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni akizungumza jambo
katika hafla uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi
wa Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ya Mikoani na
Nchi Jirani cha ubungo jijini Dar es Salaam.
Masauni
baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya usalama
barabarani inayoratibiwa na Mabalozi wa Uslama Barabarani RSA Tanzania
leo jijini Dar es Dar es Salaam.
Aliyekuwa
Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azani (kushoto) ambaye pia ni mjumbe wa
kamati ya Usalama barabarani akifatilia hotuba ya mgeni rasmi hayupo
pichani katika uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na
Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Sumatra,Gilian Ngewe akizungumza katika kampeni ya Paza Sauti
iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania leo jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa na
Kamanda Kikosi cha Usalama Babarani (DCP), Mohamed Mpinga ndani ya moja
ya mabasi katika kituo cha Mabasi ya Mikoani na Nchi Jirani cha Ubungo
katika uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa
Usalama Babarani RSA Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria katiika katika uzinduzi wa kampeni ya Paza
Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania leo
jijini Dar es Salaam.
Naibu
wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandis Hamadi Masauni (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahamasihaji wa mauala ya
ualama barabarani na viongozi wengine wa kamati za usalama barabarani.