Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wastaafu wa Taaluma ya Elimu, Profesa Herme Joseph Mosha
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wakati wa kukitambulisha rasmi
Jukwaa hilo katika Ukumbi wa Idara ya Habari –MAELEZO leo jijini Dar es
Salaam. Kutoka kushoto ni wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho Bibi.
Khadija Mchatta Maggid na Muhwela Kalinga.
Katibu
Mtendaji wa Jukwaa la Wastaafu wa Taaluma ya Elimu, Bibi. Marystella
Maufi Wassena akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kukitambulisha
Jukwaa hilo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa
hilo Profesa. Herme Joseph Mosha
Mjumbe
wa Sektretarieti ya Jukwaa la Wastaafu wa Taaluma ya Elimu Bw. Muhwela
Kalinga akielezea jambo wakati wa mkutano wa kukitambulisha chama hicho
leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Profesa
Herme Joseph Mosha.
Baadhi ya Sekretarieti ya Jukwaa la Wastaafu wa Taaluma ya Elimu wakiwa katika
mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Picha
zote na: Frank Shija
WALIMU wastaafu nchini
wameanzisha jukwaa maalum litakalotumika kwa ajili ya kushauriana na
kubadiliana uzoefu baina yao na serikali kuhusu mfumo na utaratibu utoaji bora
wa elimu nchini.
Hayo yamesemwa leo,
Jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa jukwaa hilo Prof. Herme Mosha alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari juu ya lengo la uanzishwaji wa jukwaa hilo.
Prof. Mosha alisema
walimu wastaafu wana uzoefu mkubwa katika sekta ya elimu hivyo kupitia jukwaa
hilo watakuwa wakitafakari maeneo ambayo sekta ya elimu haitoweza kufanya vizuri na hivyo kuishauri
hatua zinazopaswa kuchuliwa na Serikali.
“Unapokuwa mtumishi
wa Umma unaona kila kitu kinaenda sawa, lakini unapokuwa nje unaona kuna mambo
mengi ambayo yalikuwa hayaendi sawasawa,” alifafanua Prof. Mosha.
Kwa mujibu wa Prof.
Mosha alisema alipokuwa katika utumishi Umma walikuwa wakiandikisha wanafunzi
wa darasa la kwanza kwa asilimia 95,
lakini baada ya tamko la elimu bila ada idadi ya wanafunzi iliongezeka zaidi.
Prof. Mosha alisema
kitendo hicho kinaonyesha kuwa n kwamba
asilimia kubwa ya watoto walikuwa hawaandikishwi kuanza elimu ya msingi kutokana
na vikwazo vya ada.
Aidha aliipongeza
serikali Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kuboresha sekta ya elimu ambapo kwa sasa kila mwanafunzi anakaa katika dawati
tofauti na miaka ya nyuma.
Kwa upande wake
Katibu wa Jukwaa hilo Bi. Marystella Wassena alisema jukwaa hilo litakuwa
likijishughulisha pia na kufanya tafiti
mbalimbali za kuboresha sekta ya elimu.
Bi. Wassena aliwataka walimu waastaafu nchini kujiunga na jukwaa hilo na kutumia uzoefu walioupata ili kuishauri Serikali na kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa katika ngazi zote za elimu