Mkurugenzi
Mtendaji wa Startimes Liao Lanfang (katikati) pamoja na Meneja wa
Quality Group Utkarsh Garg (kulia) wakitia saini makubaliano ya
kuonyesha filamu ya kwanza ya Kichina katika jumba la Sinema
wakishuhudiwa na Mshauri wa masuala ya utamaduni kutoka ubalozi wa
China, Gao Wei.
Na Zainab Nyamka,
Globu ya Jamii
KATIKA
kutambua uhusiano mkubwa uliopo baina ya Tanzania na China Kampuni ya
Startimes imezindua filamu ya kichina kwa mara ya kwanza na inatarajiwa
kuonyeshwa katika Jumba la Sinema la Quality Centre.
Filamu
hiyo ijulikanayo kama Goodbye Mr Looser yenye maudhui ya kichina pamoja
na tafisri ya maandishi kwa kiswahili inakuwa ni mara ya kwanza
kuonyeshwa kwenye jumba la sinema kwa hapa nchini kwani haijawahi
kuletwa filamu za aina hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya utiaji wa saini wa mkataba huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Startimes Liao Lanfang amesema kuwa
hii ni moja ya hatua kubwa iliyofikiwa hasa baada ya kuona kuwa
watanzania wengi wanaangalia tamthilia za Kichina lakini hawajawahi
kuona filamu kutoka nchini humo na hii ni fursa kwao kuweza kuiona kwa
mara ya kwanza.
Lanfang
amesema kuwa jitihada kubwa ziliweza kufanyika kuhakikisha filamu hii
inafika nchini Tanzania na imeweza kufanikiwa nakatika filamu hii
itakayokuwa na tafsiri ya maandishi ya kiingereza itaonyeshwa kwa mara
ya kwanza kwenye Jumba la Sinema la Quality Centre.
Meneja
wa Quality Group Utkarsh Garg amesema kuwa katika jumba lao la sinema
hakujawahi kuja filamu kutoka nchini China na hii ni mara ya kwanza na
itarushwa katika jumba lao na wamefurahi sana kuweza kupata nafasi hiyo.
Mshauri
wa masuala ya utamaduni kutoka ubalozi wa China, Gao Wei amesifia kwa
hatua hii kubwa kufika hapa nchini kwani anafahamu watanzania wengi
wameshazifuatilia tamthilia za kichina kama vile Mau dodo na nyinginezo
ambazo zilikuwa zinainyeshwa katika chaneli mbalimbali zinazopatikana
katika kisimbuzi cha Startimes.
Meneja
wa Quality Group Utkarsh Garg akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya kuonyesha filanu ya kichina
kati yao na kampuni ya Startimes
Mkurugenzi
Mtendaji wa Startimes Liao Lanfang akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya kuonyesha filanu ya
kichina kati yao na jumba la sinema la Quality Centre.
Mshauri wa masuala ya utamaduni kutoka ubalozi wa China, Gao Wei akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kushuhudia utiaji wa saini ya
makubaliano ya kuonyesha filanu ya kichina katika jumba la sinema la
Quality Centre.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Startimes Liao Lanfang (kushoto) pamoja na Meneja wa
Quality Group Utkarsh Garg wakibadilishana nyaraaka za makubaliano
mara baada ya kutia saini.
Picha zote na Zainab Nyamka
No comments:
Post a Comment