Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha cha dola laki mbili za Kimarekani (USD 200,000) -takriban Tshs. 437,000,000/- taslimu
kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha ( wa
pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini
Uganda Mhe. Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda
Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa Tetemeko
la ardhi mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma taarifa kuhusu
Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Boniface Muhia mara baada ya
kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na kwa
misaada mbalimbali ya mabati 4,000 na vifaa vya majumbani ikiwemo
magodoro na mashuka ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka
Kenya muda wowote kuanzia sasa. Katikati ni Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa fedha dola laki mbili za
Kimarekani (takriban Tshs. 437,000,000/- )
taslimu kutoka Uganda pamoja na taarifa ya Tetemeko la ardhi
lililotokea mkoani Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment