Michezo : Serengeti Boys yaibamiza Congo Brazaville 3 - 2 Uwanja wa Taifa Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


18 Sep 2016

Michezo : Serengeti Boys yaibamiza Congo Brazaville 3 - 2 Uwanja wa Taifa Jijini Dar

 Ankal na mtangazaji Mkongwe Abdallah Majura walikuwepo kushuhudia  Serengeti Boys wakicheza dhidi ya Congo Brazaville wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani. Nyuma yao ni Kanali Mstaafu Iddi Kipingu
Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mh.Ibrahim Raza na familia yake walikuwepo pia 
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  na wadau wa michezo wakiwa jukwaa juu.
 Kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa "Master" akiangalia madini mapya
 Mmoja wa viongozi wa timu ya Congo Brazaville akishangilia 
 Ankal akiwa na mweka hazina msaidizi wa Kariakoo Family Development Foundation (KFDF) uwanjani
 Timu zikiwa uwanjani kabla ya mchezo
 Wimbo wa Taifa
 Furaha ya ushindi
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wachezaji wa Serengeti Boys na waandishi wa habari  Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville 

TIMU ya Serengeti Boys imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Congo Brazaville katika mchezo wa kufuzu kuingia fainali za mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Madagascar  uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo ulioanza kwa kasi na kila upande kushambuliana kwa zamu zilianza kuzaa matunda kwa timu ya Serengeti Boys kuandika goli la kwanza dakika ya 38 liliolofungwa na Yohana Mkomola na dakika ya 42 akafanikiwa kuongeza goli la pili kwa Serengeti Boys.

Mpaka inafikia mapumziko Serengeti Boys walikuwa mbele kwa goli 2-0 lakini dakika ya 73, Langa-Lesse Percy anaiandikia Congo Brazzaville goli la kwanza kwa mkwaju wa penati baada mchezaji kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Issa Makamba anaipatia Serengeti Boys goli la tatu akitumia nafasi nzuri aliyoipata lakini halikudumu sana katika dakika ya 90 Poboumela Chardon akaipatia Congo Brazzaville goli la pili kwa kutumia uzembe wa goli kipa Kelvin Kayego aliyeingia kuchukia nafasi ya Ramadhan Kabwili aliyeumia wakati akiokoa penati.

Mpaka mpira unamalizika Serengeti Boys wametoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 3-2.

Kila timu iliweza kufanga mabadiliko na kwa upande wa Serengeti Boys walimtoaYohana Mkomola na kuingia Issa Makamba, Ibrahim Ali na kuingia Muhsin Makame na kwa Congo Brazaville alitoka Mboungou Prestige na kuingia Mountou Edoward, Mantourari Aldo na kuingia Makoina Beni na Kiba Konde Rodrique na kuingia Bopoumela Chardon.
 Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Vijana "Serengeti Boys", Yohana Oscar Mkomola akikimbilia upande walipo mashabiki mara baada ya kuipatia timu yake Goli, katika Mchezo wao dhidi ya Congo Brazaville wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani. Serengeti Boys imeibuka na ushishi mwembamba wa bao 3-2, hivyo watajipanga kwa mchezo wa marudiano utakaochezwa juma lijalo. Magoli ya Serengeti Boys yamefungwa na Yohana Oscar dakika ya 38 na 42 na Issa Abdi Makamba dakika ya 70, huku magoli ya Congo Brazaville yakifungwa na Langa-Lesse Percy kwa mkwaju wa penani na dakika ya 90 Poboumela Chardon.
 Mabeki wa Timu ya Congo Brazaville wakiusindikiza kwa macho mpira uliopigwa vizuri kabisa na Mchezaji wa Serengeti Boys, Issa Abdi Makamba na kuipatia timu yake bao la tatu, katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani.
 Beki wa Timu ya Taifa ya vijana ya Congo Brazaville, Moundza Prince akiwa ameruka juu kuondosha hatari iliyokuwa imeelekeswa langoni kwake, katika mchezo dhidi ya Serengeti Boys uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
 Mchezaji wa Timu ya Congo Brazaville akionyesha uwezo wake wa kuzuia mpira.
 Beki wa Timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ally Hussein Msengi akizuia shambulizi lililokuwa likielekezwa langoni kwake na Mshambuliaji wa Congo Brazaville, Mboungou Prestige, katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani. Serengeti Boys imeibuka na ushindi mwembamba wa bao 3-2.

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Vijana "Serengeti Boys", Asad Juma akichuana vikali na Mpinzani wake Mboungou Prestige wa Timu ya Congo Brazaville, katika mchezo dhidi ya Serengeti Boys uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.


Post Top Ad