Wataalamu
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa wamewasili nchini India
kwa ajili ya kujengewa uwezo wa kupandikiza figo kwa wagonjwa wenye
matatizo ya figo. Wataalamu hao watakuwapo India kwa muda miezi mitatu
na watarejea nchini Desemba 10, mwaka huu.
Mkurugenzi
wa Tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Hedwiga Swai
akizungumza baada ya wataalamu hao kwenda India kwa ajili ya kujengewa
uwezo wa upasuaji na upandikizaji figo.
Mkuu
wa Idara ya Urolojia katika hospitali hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro
akizungumza na wataalamu wenzake kabla ya kuanza kwa safari ya kuelekea
India.
Mkuu wa Idara ya Urolojia katika hospitali hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro akizungumza na wenzake kabla ya kuondoka nchini.
Baadhi
ya wataalamu wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Urolojia katika hospitali
hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro wakati akitoa maelezo kabla ya kuanza safari
ya kuelekea India wiki iliyopita.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Na John Stephen, MNH.
Dar es
Salaam, Tanzania. Wataalamu 20 wa fani mbalimbali wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) wameondoka nchini kwenda India kwa ajili ya
kujengewa uwezo wa upandikizaji figo kwa watu wenye matatizo ya figo.
Wataalamu
hao wameondoka wiki iliyopita na wakiwa huko watajengewa uwezo wa
kufanya upasuaji na upandikizaji figo kwa wagonjwa wenye matatizo ya
figo.
Mkurugenzi
wa Tiba, Dk. Hedwiga Swai amesema leo kwamba wataalamu mbalimbali
wakiwamo madaktari bingwa wa upasuaji na upandikizaji figo, madaktari
bingwa wa magonjwa ya figo, wataalamu wa maabara, madaktari wa usingizi
na madaktari wa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Wengine
ni wataalamu wa mionzi, wauguzi wa chumba cha upasuaji na chumba cha
wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na wataalamu wengine ambao
wanakwenda kujifunza.
“Suala
la mgonjwa kupandikizwa figo ni mchakato na haliwezekani kufanywa na
mtaalamu mmoja.Ni kazi inayowahusisha wataalamu wengi,” amesema Dk.
Swai.
Pia,
Dk. Swai amesema upandikizaji figo utapunguza rufaa za wagonjwa kwenda
nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kuokoa fedha nyingi za
serikali za kuwapeleka nje ya nchi.
Amesema kwamba wataalamu hao watakaa nje ya nchi kwa muda wa miezi mitatu na watarejea nchini Desemba 10, 2016.
“Shughuli za upasuaji na upandikizaji figo zitaanza Januari mwakani,” amesema Dk. Swai.
No comments:
Post a Comment