Usalama Barabarani : Kamanda Mpinga Atoa Elimu ya Usalama Barbarani kwa Madereva wa Bodaboda - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Sept 2016

Usalama Barabarani : Kamanda Mpinga Atoa Elimu ya Usalama Barbarani kwa Madereva wa Bodaboda


Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania, mohammed Ramadhan Mpinga, akitoa elimu ya usalama bararani kwa waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 kutoka kundi E, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania, mohammed Ramadhan Mpinga, akitoa elimu ya usalama bararani kwa waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 kutoka kundi E, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).
Msaidizi wa Kamanda DCP Mpinga, SACP Fortunatus Muslim, akitoa elimu ya usalama bararani kwa waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 kutoka kundi E, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.
S/SGT Enock Machunde, Kitengo cha Elimu kutoka Traffic Makao Makuu Dar es Salaam, akitoa elimu ya usalama bararani kwa wachezaji wa timu zilizoshiriki kundi E ambao ni waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).


PC Abdallah Ismail, Kitengo cha Elimu kutoka Traffic Makao Makuu, akitoa elimu ya usalama bararani kwa wachezaji kabla ya kuingia Uwanjani wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 yanayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).
Mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki kutoka mkoa wa Kipolisi Ilala, Mademla Bang’ala, akifafanua jambo kabla ya michezo hiyo kwenye michezo ya kundi (E) timu za waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).


Na: Uswege John Mwaisemba

Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania, Mohammed Ramadhani Mpinga, Juzi alikuwa ni miongoni mwa Wakufunzi wa kutoa elimu ya Masuala ya Usalama Barabarani wakati wa mashindano ya Mpinga Cup 2016 yanayohusisha madereva wa Pikipiki na bajaji kwa mkoa wa Kipolisi wa Ilala jijini Dar es Salaam katika mfululizo wa michezo hiyo inayoendelea katika viwanja mbalimbali.

Katika mashindano hayo jumla ya timu 59 tayari zimefanikiwa kusonga mbele hatua ya pili ya mtoano wa mashindano haya ambayo mwishoni mwa wiki timu zilizocheza zilikuwa ni pamoja na Matunda fc dhidi ya Zahanati ambapo mashindi alikuwa ni zahanati ,alipatikana kwa njia ya penalt 5-4, wafungaji kwa upande wa Zahanati wakiwa ni Fredy Chambogo, Isaac Elisha, Musa Masho, Shiiko Rashifod , na mfungaji wa timu ya Matunda walikuwa ni Shaaban Awami, Kelvin Sweetbati, Salum MWaikimba, Yusuph Mohamed.

mchezo wa pili ulikuwa ni Kwa bibi fc aliyecheza na Chama fc na Mshindi alikuwa ni Chama Fc kwa jumla ya 1-0, mfungaji akiwa Amani kadodo dakika ya 18 kipindi cha kwanza, mchezo wa tatu ulizikutanisha timu za Tabata Bodaboda na Tabata Old Trafford na mshindi alikuwa ni timu ya Tabata Bodaboda kwa jumla ya mabao 3-1 wafungaji kwa upande wa Traffod walikuwa Abdallah Hussen dk 27 kipindi cha kwanza, Miraji Sarehe dk 36 kipindi cha kwanza na goli la tatu liliwekwa kimiani na Saidi Ngwira katika dakika za majeruhi.

Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya Barakuda Kilimanjaro na Barakuda Fc ambapo mshindi alikuwa ni timu ya Barakuda Kilimanjaro kwa ushindi wa mezani baada ya wapinzani kushindwa kutokea uwanjani. Na mchezo uliofuata ulikuwa ni kati ya timu ya Liwiti fc dhidi ya Luwi Safari fc ambapo mchindi alikuwa ni timu ya Liwiti fc waliopata ushindi wa chee baada ya wapinzani kushindwa kutokea uwanjani.

Timu zilizofuatia katika ku hiyo ya jumamosi ilikuwa ni kati ya Kinyerezi Saloon waliocheza na Mbuyuni Fc ambapo matokeo katika mchezo huo timu ya mbuyuni waliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 mfungaji akiwa Kitenge Kitenge aliyefunga dakika ya 16 kipindi cha kwanza na mchezo uliofuata ulizikutanisha timu za Segerea SBG dhidi ya timu ya Segerea Sheli Bodaboda na matokeo katika mchezo huo timu ya Segerea Sheli Bodaboda waliibuka mshindi wa 1-0 mfungaji akiwa Jackson Hamadi dakika 25 kipindi cha pili.

Mashindano hayo yaliendelea tena siku ya jumapili ambapo jumla ya timu kumi na mbili zilishiriki kuwania nafasi ya kusonga mbele na mchezo wa kwanza ulikuwa ni kati ya Transpoter Fc iliyocheza na Kecha Fc na Timu ya Kecha ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mfungaji katika mchezo huo akiwa ni Mashaka Hamisi aliyefunga kwa shuti kali dakika 18 ya kipindi cha ili, huku ukifuatiwa na mchezo kati ya White Egle fc dhidi ya timu ya Migombani Fc ambapo mchezo huo timu ya White Egle iliibuka na ushindi wa mabao 8-7 baada ya kupigiana penalt kutokana na timu hizo kushindwa kutambiana kwenye dakika 90 za mchezo baada ya kumaliza zikiwa zimefungana bao 1-1.

Wafungaji kwa timu ya White Egle walikuwa ni Selemani Uswege, Elick Fod, Muso Uswege, Zuberi Hassani, Jofu Tito, Erick Sabuni, wafungaji kwa upanda timu ya Migombani walikuwa ni Shaaban Hamisi, Juma Abdalah, Erick Ndidi, Sifaeli Haule, Patrick Esau, Hamadi Msuyale na Dua Juma.

Akizungumzia mashindano hayo Mratibu wa mashindano ASP Mbuja Saidi Matibu alisema kuwa, mpaka sasa mashindano hayo yanaendelea vizuri na amewapongeza viongozi wa tmu kwa kuweza kufika kwa wakati kwenye michezo yao na kwamba timu zote zimeshiriki na kukubali matokeo kwa timu zote zilizofungwa, na pia wachezaji wamekuwa na hamasa ya hali ya juu na kuomba mashindano haya kuwa endelevu, ili kuwafikia bodaboda kwa wingi ikiwezekana iwe kwa nchi nzima.

Nae Mwenyekiti wa bodaboda mkoa wa Kipolisi Ilala, Mademla Bang’ala alisema kuwa, wanamshukuru kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani kwa niaba ya Jeshi la Polisi kwa kuwapa changamoto madereva wa bodaboda kwa kujenga afya zao kwa njia hiyo ya michezo na kuwapa elimu ya Usalama barabarani ili kuepukana na ajali za mara kwa mara, na kwamba wanaomba mashindano haya yasiishie tu mkoa wa Dar es salaam na badala yake yapelekwe kwenye Mikoa yote ya Tanzania.

Mchezo mwingine ulikuwa ni Buguruni sheli fc Bodaboda waliocheza na timu ya Buguruni Sheli Bajaji mshindi katika mchezo huo alikuwa ni timu Buguruni Sheli bajaji kwa jumla ya mabao 3-1,wafungaji kwa upande wa timu ya bodaboda ni Willy Pashau na kwa upande wa Bajaji wafungaji ni Abdul Ismail, moshi Shilingi, na Chrispofe Chibondo, mchezo mwingine uliofuata siku ya jumapili ulikuwa ni kati ya timu Segerea Mangala Fc waliocheza na timu ya Sanene fc na mshindi alikuwa ni timu ya Segerea Mangala fc kwa njia ya matuta 3-1 wafungaji kwa uande wa Segerea mangala ni Abeid Musa, Amani Saidi, Mbonde Ashilafu, baada ya kumaliza dakika 90 timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa mabao 4-2 na wafungaji kwa upande wa timu ya Sanene fc walikuwa ni Samba John na Mrisho Issa.

Wakati huo huo Afisa habari Msaidizi wa timu za bodaboda Tito Razalo Mpiziwa amemshukuru kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani kwa kuweza kufanikisha mashindano haya, ambayo kwa muonekano tayari ni zaidi ya bodaboda 6000 wa mkoa wa Dar es salaam walioweza kunufaika na mashindano haya kutokana na kupata mafunzo ya elimu ya usalama barabarani.

Mchezo mwingine ulizikutanisha timu za Kwetu pazuri fc na Segerea Kona Fc ambapo mshindi alikuwa ni timu ya Kwetu Pazuri waliopata ushindi wa mezani baada ya wapinzani wao kushindwa kutokea uwanjani , na mchezo uliofuata ulikuwa ni kati ya Pelalela fc waliocheza na timu ya Relini kwa Mnyamani na mshindi alikuwa ni Timu ya Relini kwa Mnyamani waliopata ushidi wa bure.



Mashindano haya yanadhaminiwa na Baraza la Usalama Barabarani(T), Jeshi la Polisi Tanzania, Cool Blue Tanzania, NMB, Zantel, Reb Bull, Windhoeck, Coc cola, Haki Elimu, Star Times, EFM Radio, Michuzi Blogs, NHIF, BIG BON, GSM, T-Marc Tanzania, Bavaria, Chai Bora, Dar City Promotions, Yono, Mwananchi Communications, Quality Group, Puma, TBL, Milcom, My Way Entertainments, Balozi wa Demokrasia Tanzania, Miss Demokrasia Tanzania, na MpaluleBlogs.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad