Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini,
Profesa James Mdoe amekitaka Kitengo cha Dharura cha Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO) kufanya kazi kwa ubunifu ili kukabiliana na malalamiko
ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi mara kwa mara.
Profesa
Mdoe aliyasema hayo mara baada ya kufanya ziara katika banda la Wizara
ya Nishati na Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya
Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuwa malalamiko ya wananchi juu ya ucheleweshaji wa huduma
unaofanywa na kituo cha dharura cha TANESCO yamepelekea wananchi kuwa
na taswira hasi juu ya shirika hilo.
“Ninawataka
kuwa wabunifu katika utendaji kazi wenu, kwa kutoa huduma kwa haraka
kwa kuwa nyinyi ndio mliobeba taswira ya shirika,”alisema Profesa Mdoe.
Wakati
huo huo akizungumzia sekta ya madini nchini, Profesa Mdoe alisema kuwa
Serikali imejipanga katika kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini
kwa kuwa wana mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Alisema
kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (SMMRP),
Serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo wa madini
wanaokidhi vigezo.
Alitaja
vigezo hivyo kuwa ni pamoja na kuwa na leseni za uchimbaji madini,
kuonesha kuwa wanaendesha shughuli za uchimbaji madini pamoja na ulipaji
wa kodi serikalini.
Alisisitiza
kuwa Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ipo
tayari kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa kuwapatia vifaa na mafunzo ili
kukuza uzalishaji wa madini nchini na hivyo sekta hiyo kuwa na mchango
mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi
Mtaalam
kutoka Kampuni ya Kuendeleza Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC),
Mhandisi Nyaso Makwaya (kulia) akielezea shughuli za kampuni hiyo kwa
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Madini Prof. James Mdoe (wa pili kutoka kushoto) mara alipotembelea
banda la TGDC.
Mtaalam
kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini Philip Mathayo
(kushoto) akitoa maelezo juu ya sera ya madini kwa Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe
(wa pili kutoka kulia) mara baada ya kuwasili kwenye banda la Wizara
kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika katika viwanja
vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam
kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Marwa
Petro (kushoto) akielezea sera ya nishati kwa Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe
(wa pili kutoka kulia) mara baada ya kuwasili kwenye banda la Wizara
kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika katika viwanja
vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia kabisa ni Kaimu Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara, Asteria Muhozya.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini
Prof. James Mdoe ( wa kwanza kulia) akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kupata maelezo kutoka kwenye banda hilo.
Afisa
Uhusiano wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Yasin Silayo (kushoto)
akielezea majukumu ya shirika hilo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kulia).
Afisa
Mawasiliano kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA)
Mhandisi Yisambi Shiwa (kulia) akielezea majukumu ya wakala huo kwa
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Madini Prof. James Mdoe (kushoto) mara alipotembelea banda la wakala
huo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini
Prof. James Mdoe (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili katika banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) Zena Kongoi (kulia)
akielezea mikakati ya shirika hilo katika kuwasaidia wachimbaji wadogo
kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Madini Prof. James Mdoe (kushoto)
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini
Prof. James Mdoe (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada
ya kutembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake.
Meneja
Uendelezaji Masoko na Teknolojia kutoka Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) Mhandisi Advera Mwijage (kulia) akimwonesha Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe
(katikati) matumizi ya majiko sanifu katika kupikia mara alipotembelea
banda la REA. Kushoto kabisa ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Asteria Muhozya.
Mtaalam
kutoka kampuni ya Arti Energy ambayo ni mdau wa Walala wa Nishati
Vijijini (REA), Abdallah Seushi (kulia) akielezea bidhaa zinazosambazwa
na kampuni hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto) mara alipotembelea
banda la REA.
Afisa
Maendeleo ya Jamii kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini
(TPDC), Ally Mluge (kulia) akielezea muundo wa shirika hilo kwa kwa
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Madini Prof. James Mdoe (kushoto) mara alipotembelea banda la TPDC.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini
Prof. James Mdoe akiangalia kombe la ushindi wa kwanza kwenye kundi la
makampuni ya gesi na mafuta la Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini
(TPDC) kwenye banda lake.
No comments:
Post a Comment