Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest
Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
Frank Charles Msaki kutokana na makosa ya kufanya malipo hewa yaani
kulipa posho ya chakula kwa watu ambao si askari.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka Wizarani hapo ambayo nakala tumeipata, Mhasibu
Mkuu huyo Bw. Frank Msaki anasimamishwa kazi kwa kufanya malipo ya
kiasi cha sh. 305,820,000 kama posho ya chakula kwa watu ambao sio
askari kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
Meja
Jenerali Rwegasira amesema kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za
Kijeshi anayetakiwa kulipwa posho ya chakula yaani ‘ration allowance’
ni askari peke yake na si mtu mwingine yeyote yule.
Meja
Jenerali Rwegasira amesema anamsimisha kazi Mhasibu Mkuu huyo tangu leo
tarehe 9 Julai, 2016 ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya tuhuma
zinazomkabili.
Katibu
Mkuu huyo amesema baada ya jalada la uchunguzi kufunguliwa na Ukaguzi
Maalumu kufanywa na Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi imebainika kuwa
mbinu mbalimbali zimetumika ili kufanikisha malipo hayo hewa.
No comments:
Post a Comment