Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba, (pichani katikati), akimpatia maelezo mwananchi huyu
Tobist Machenje, (kulia), wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Fulgence Sebera.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, ametembelea mabanda ya wadau wa Mfuko huo ili kubadilishana mawazo na kuelewa shughuli za wadau hao, kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Sambamba na kutembelea mabanda hayo Mshomba pia aliungana na wafanyakazi wake, katika kutoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la WCF na kuwaeleza shughuli za Mfuko huo ulioanzishwa mwaka mmoja uliopita na ushiriki wa maonyesho hayo ni wa kwanza kwa Mfuko huo.
Miongoni mwa mabanda aliyotembelea Mkurugenzi huyo ni pamoja na lile la Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Chama cha Waajiri Tanzania, (ATE), Mfuko wa Pensheni wa PSPF, GEPF, na UTT-PID. Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ulianzishwa kwa sheria namba 20 ya mwaka 2008 iliyorejewa mwaka 2015 ya Fidia Kwa Wafanyakazi. Na kazi kubwa ya Mfuko huo ni kutoa Fidia kwa Mfanyakazi aliyeumia au aliyepata magonjwa wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi
Wafanyakzi wa WCF wakiwa kwenye banda la Mfuko huo, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Edward Kerenge, Zaria Mmanga, na Aly Sheha
Afisa wa Fedha wa WCF, Edward Kerenge, (kulai), akiwapatia maelezo wananchi waliofika kwenye banda la Mfuko huo
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakiongozwa na Meneja Masoko na Uhusiano Costantina Martin, (watatu kushoto). Wakwanza kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera
Mshomba(kulia), akisindikizwa na Meneja Masoko na Uhusiano wa PSPF, Costantina Martin, baada ya kutembelea banda la Mfuko huo
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (katikati), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba, (kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera, wakati Mshomba kutembelea banda la PSPF
Mshomba akitembelea banda la UTT-PID
Mshomba akisalimiana na wafanyakazi wa GEPF alipotembelea banda lao
Mshomba akipitia jarida la Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), huku akipatiwa ufafanuzi na Meneja wa huduma za Kisheria wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran, wakati alipotembeela banda la ATE. Kulia ni Mratibu wa mradi wa NHO, Joyce Nangai
Mshomba akizungumza jambo na Suzanne Ndomba-Doran
Mshomba akitembeela banda la OSHA
Mshomba akiuliza kitu kwa maafisa hawa wa UTT-PID alipotembelea banda la taasisi hiyo
Edward Kerenge, akiwapatia maelezo wananchi hawa waliotembelea banda la WCF
Afisa Uhusiano wa WCF, Zaria Mmanga, (kulia), akimpatia maelezo, mwananchi huyu aliyefika banda la Mfuko huo kujua shughuli zake
Afisa wa Fedha wa WCF, Grace Tarimo, (kulia), akimpatia amelezo ya shughuli za Mfuko, mwananchi huu aliyetembelea banda la Mfuko kujua kazi zake
Afisa wa Fedha wa WCF, Grace Tarimo, (kulai), akimpatia
amelezo ya shughuli za Mfuko, mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko
kujua kazi zake.
No comments:
Post a Comment